Breaking

Thursday, 30 November 2023

MAHAFALI YA 53 YA CHUO KIKUU CHA DAR ES SALAAM

NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM

MAKAMU Mkuu wa Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam, Prof. William Anangisye amewataka wahitimu kutumia elimu kubwa walioipata kuleta ushawishi chanya kwa watu wote wanaowazunguka kwani elimu walioipata ni mali ya Umma hivyo basi elimu lazima ilete faida.

Aidha amewataka wahitimu wawe wazalendo kwa nchi yao kwani watu wengi wanatarajia mengi kutoka kwao “hakuna mtu mwenye akili timamu asiyetambua mchango wa vijana wanaojitambua katika kuendeleza familia, Jamii na Taifa lao”. 

Wito huo ameutoa leo Novemba 30,2023 wakati wa Mahafali ya 53 ya Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam yaliyofanyika katika Ukumbi wa Mlimani City Jijini Dar es Salaam.

Prof. Anangisye amewaeleza wahitimu kuwa endapo ajira Serikalini au katika sekta binafsi zitachelewa kupatikana wawe wepesi kuangalia sehemu nyingine ambapo maarifa na ujuzi wao unaweza kutumika kwa ufanisi zaidi.

Pamoja na hayo amesema kuwa ndani ya mwaka mmoja kimepiga hatua muhimu ya Maendeleo ikiwemo kuandaa Kongamano la Kwanza la Kiswahili nchini Ghana lililofanyika kwa kushirikiana na Chuo Kikuu Cha Ghana-Legon.

Amesema kuwa kwenye Mafanikio hayo pia Chuo, kimefanikiwa kukamilisha ujenzi wa jengo la kutolea huduma katika kituo cha Afya ili kuwapatia wanajumuiya ya Chuo huduma bora za afya.

Ameeleza kuwa  Chuo kimeendelea kuunga mkono juhudi za Serikali za kuendeleza lugha ya Kiswahili ndani na nje ya mipaka ya Tanzania ambapo Chuo kilisaini Mkataba wa Makubaliano wa kufundisha Kiswahili na Chuo Kikuu Cha Havana kilichoko Cuba.
Mkuu wa Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam, Rais Mstaafu Dkt.Jakaya Kikwete akiwatunu Shahada za Uzamili, Awali, Stashahada na Astashahada wahitimu kwenye Mafahali ya 53 ya Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam yaliyofanyika leo Novemba 30,2023 Jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam, Rais Mstaafu Dkt.Jakaya Kikwete akiwatunu Shahada za Uzamili, Awali, Stashahada na Astashahada wahitimu kwenye Mafahali ya 53 ya Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam yaliyofanyika leo Novemba 30,2023 Jijini Dar es Salaam.
Naibu Makamu Mkuu wa Chuo-Taaluma, Prof. Bonaventure Rutinwa akisoma hotuba katika Mafahali ya 53 ya Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam yaliyofanyika leo Novemba 30,2023 Jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Baraza la Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam, Balozi Mwanaidi Sinare akiteta jambo na Naibu Makamu Mkuu wa Chuo- Mipango, Fedha na Utawala, Prof. Bernadeta Killian katika Mafahali ya 53 ya Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam yaliyofanyika leo Novemba 30,2023 Jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Baraza la Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam, Balozi Mwanaidi Sinare akisoma hotuba katika Mafahali ya 53 ya Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam yaliyofanyika leo Novemba 30,2023 Jijini Dar es Salaam.
Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam, Prof. William Anangisye akisoma hotuba katika Mafahali ya 53 ya Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam yaliyofanyika leo Novemba 30,2023 Jijini Dar es Salaam.
Wahitimu wakiwa kwenye Mahafali ya 53 ya Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam yaliyofanyika leo Novemba 30,2023 kwenye Ukumbi wa Mlimani City Jijini Dar es Salaam
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: +255 621 896 990

Pages