Breaking

Thursday, 9 November 2023

WAZIRI WA NISHATI ZANZIBAR AWAPONGEZA WANAJIOSAYANSI KWA KAZI KUBWA WANAYOIFANYA

Waziri wa Nishaji, Maji na Madini Zanzibar, Mhe. Shaib Hassan Kaduara amewapongeza wanajiosayansi nchini kwa kazi kubwa wanayofanya katika kutafuta rasilimali mbalimbali zikiwemo madini, mafuta na gesi asilia, joto ardhi na maji ya ardhini.

Kaduara ametoa pongezi hizo leo Novemba 09, 2023 Mjini Unguja wakati akifungua mkutano wa wanajiosayansi kwa niaba ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi,

Akizungumza katika mkutano huo, Kaduara amesema kuwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar inatambua na kuthamini mchango wa wanajiosayansi katika kutimiza ajenda ya uchumi wa buluu na kufikia Dira ya Maendeleo ya Zanzibar 2050.

"Kada ya jiosayansi ni muhimu sana katika utafutaji na uendelezaji wa rasilimali mbalimbali zikiwemo madini, mafuta na gesi asilia, maji ya ardhini, joto ardhi nakadhalika. Nitumie fursa hii kutoa rai kwenu wanajiosayansi kutumia taaluma yenu kwa weledi kwani, kama niliyosema awali, taaluma hii ina mchango mkubwa sana katika kifikia Dira ya Maendeleo ya Zanzibar 2050", alieleza Mhe. Kaduara.

Kaduara pia amezipongeza Wizara ya Madini ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Wizara ya Nishati, Maji na Madini ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa kuwa walezi wa Jumuiya ya Wanajiosayansi Tanzania.
Waziri wa Nishaji, Maji na Madini Zanzibar,  Mhe. Shaib Hassan Kaduara akifungua Mkutano wa Wanajiosayansi Tanzania ulioanza leo Novemba 09, 2023 katika Hoteli ya Golden Tulip Zanzibar.
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: +255 621 896 990

Pages