Akizungumza wakati wa kufunga mafunzo Mheshimiwa Mkuu wa wilaya ametoa pongezi na shukrani kwa viongozi wa kata ya Idukilo kwa kuhakikisha mafunzo ya jeshi la akiba "Mgambo" yameanza na kumalizika salama, Pia amewashukuru Wakufunzi waliohusika kutoa mafunzo na kuwafanya wanafunzi kuhitimu mafunzo hayo kwa viwango vinavyohitajika.
" Ninawapongeza na kuwashukuru sana wakufunzi wote mliotoa mafunzo haya ya viwango vinavyohitajika, wahitimu wote mkawe mstari wa mbele katika kuilinda, nchi yenu na kuwa mstari wa mbele kujitolea kazi mbalimbali za ujenzi wa Taifa,
Vilevile mafunzo mliyoyapata yakawe ni sehemu ya kupeleka elimu kwa jamii juu ya maadili mema, ikiwa ni pamoja na kushirikiana na vyombo vya Ulinzi na usalama katika kutoa taarifa za uhalifu popote pale unapotokea." Alisema Mkude
Aidha Mheshimiwa Mkude ametoa wito kwa makampuni yote ya ulinzi wilayani kuajiri vijana waliopitia katika mafunzo ya Jeshi la Akiba (Mgambo) na kuwapa kipaumbele katika nafasi za Jeshinla Kujenga Taifa ( JKT ).
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Kishapu Ndugu. Emmanuel Johnson amewapogeza sana wahitimu pamoja na wakufunzi kwa kumaliza salama mafunzo pamoja na kuahidi kutenga bajeti kupitia Mapato ya ndani kwaajili ya sare za Jeshi la akiba
Naye Kamanda wa Jeshi la Polisi Wilaya ya Kishapu Bi. Esther Gesogwe Amewataka wahitimu wote kuhakikisha usalama maeneo yote amabayo watakuwepo na kushirikiana kwa ukaribu na Jeshi la Polisi pamoja na kuimarisha Amani.




