Afisa Maendeleo ya Jamii, Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) ndugu Elizabeth Eusebius akitoa elimu kwa wananchi wa Kata ya Gezaulole katika wilaya ya Kigamboni kuhusu faida za mradi na nafasi ya wananchi wakati wa utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa mitambo ya kisasa ya kuchakata takatope inayotekelezwa katika maeneo yao.
DAWASA imeanza utekelezaji wa Ujenzi wa Mitambo ya kuchakata takatope katika Wilaya ya Kigamboni, Temeke, Ilala, Kinondoni na Ubungo.
Mradi huo utahusisha ujenzi wa mitambo 8 ya kisasa ya kuchakata takatope na utahudumia wananchi takribani Milioni moja na laki saba katika mkoa wa Dar es Salaam.
Mradi utatekelezwa kwa kipindi cha muda wa miezi 18 chini ya Mkandarasi Shanxi na Mkandarasi msimamizi Kampuni ya DOHWA.