Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Mipango na Uwekezaji, Prof. Kitila Mkumbo (Mb.) amewahamasisha wawekezaji wa Tanzania kuendelea kutumia fursa za uwekezaji na biashara zinazojitokeza kutokana na utekelezaji wa sera ya demkorasia ya uchumi.
Ameyasema hayo leo tarehe 08 Oktoba, 2023 nchini India alipokutana na sekta binafsi ya Tanzania jijini New Delhi ikiwa ni siku moja kabla ya kufanyika kwa Kongamano la biashara kati ya Tanzania na India
Kongamano hilo litafunguliwa rasmi na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe.Dkt. Samia Suluhu Hassan, linatarajiwa kuhudhuriwa na washiriki zaidi ya 250 kutoka sekta binafsi za India na Tanzania.
Mheshimiwa Waziri Mkumbo, amewahamasisha wawekezaji wa Tanzania kutumia ipasavyo ushirikiano na uhusiano wa kihistoria iliopo kati ya India na Tanzania.