Wananchi mbalimbali wamejitokeza katika ofisi za Mkoa wa kihuduma DAWASA Mivumoni kupata vifaa vya maunganisho mapya ya huduma ya majisafi baada ya kukamilisha taratibu za awali za kuomba huduma na wanategemea kuhudumiwa kupitia mradi wa maji wa Chuo kikuu hadi Bagamoyo uliokamilika mapema Mwezi Machi ,2023.
Akizungumza wakati wa kugawa vifaa hivyo, Meneja wa DAWASA -Mivumoni ndugu Gilbert Massawe amewaeleza wakazi hao kuwa kila mmoja atapata huduma na kuwasihi waendelee kujitokeza kadri ya utaratibu utakavyopangwa ili kuendelea kuchukua vifaa vya maunganisho.
"Leo tutagawa vifaa kwa wananchi takribani 250 ambao walishakwisha fanya malipo yao, hii inaashiria kuwa wanaenda kupata huduma ya Majisafi kutoka DAWASA”. ameeleza ndugu Massawe.
"Nitoe wito kwa wateja kuendelea kuongeza ushirikiano na Mamlaka na pindi wanapopata huduma kuanza kulipia ankara kwa wakati Ili wananchi wengine katika maeneo tofauti wapate huduma pia”. ameeleza ndugu Masawe
Ndugu Ramadhan Maulid mkazi wa Mivumoni ameishukuru Mamlaka kwa kuwapatia vifaa vya maunganisho na sasa wanapata uhakika wa huduma ya maji waliyoisubiri Kwa muda mrefu.
"Maeneo yetu kwa muda sasa tulikosa huduma ya maji, tunapongeza jitihada za DAWASA katika ukamilishaji wa miradi lakini zaidi kuwaunganisha wateja na huduma, leo hii tuna uhakika tunaenda kupata huduma ya maji kila mmoja katika makazi yake”.ameeleza ndugu
wakazi watakaopata huduma ni kutoka maeneo ya *Kilimahewa ,Salasala, Goba, Madale, Nyakasangwe, Muungano, Tegeta A, Mivumoni, Kulangwa, Kinzudi, Kilimahewa Juu na Boko Dovya*.
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: +255 621 896 990
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: + 255 621 615 613 au +255 621 896 990