Breaking

Thursday, 5 October 2023

WANANCHI SIHA TUNZENI NA KULINDA MIRADI YA MAENDELEO

Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM ) Mkoa wa Kilimanjaro Ndugu Komredi Patrick Boyisafi amewataka wananchi wa Jimbo la Siha kuhakikisha wanatunza miradi ya maendeleo iliyo wekezwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan ili kuweza kudumu kwa muda mrefu.

Komredi Boyisafi ametoa wito huo katika mkutano wa hadhara na wananchi wa jimbo la Siha mara baada ya kukagua utekelezaji wa Ilani katika jimbo hilo katika kata ya NgaraNairobi.

Amesema kuwa Dkt. Samia ametekeleza hilani kwa kiasi kikubwa hivyo ni wajibu wawananchi wa jimbo hilo kuhakiksha wanalinda na kutunza miradi hiyo ili kuleta tija wananchi na kizazi kijacho.

Aidha Komredi Boyisafi amempongeza Mbunge wa Jimbo la Siha Dkt. Godwin Mollel kwa kushirikiana na watendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Siha kusimamia miradi ya maendeleo na kuhakikisha matokeo chanya ya utekelezaji unaleta tija kwa wananchi

“Nakupongeza sana Mbunge Dkt. Mollel kwa kazi nzuri unayofanya katika halmashauri ya Wilaya ya Sian na mkoa wa Kilimanjaro umetia fola kwa mabadiliko makubwa yenye kuleta tija katika jamii na taifa kwa ujumla”, ameupongeza Komredi Boyisafi

Naye Mbunge wa Jimbo la Siha Dkt. Godwin Mollel amemshukuru Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM ) Mkoa wa Kilimanjaro Ndugu Komredi Patrick Boisafi kwa kusimamia Ilani ya CCM na kuhakiksha imetekelezwa kikamilifu katika jimbo la Siha.

Dkt. Mollel amesema kuwa kwa miaka miwili ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan halmashauri ya Wilaya ya Siha imepatiwa kiasi cha milioni 43.

“Komredi Boyisafi nikuhakikishie kuwa fedha hizo zimetekeleza miradi mbalimbali ikiwemo shule katika kata zetu za jimbo la Siha, uboreshaji wa miundombinu ya barabara, ujenzi wa zahanati na hospitali ya wilaya na miradi hii imetekelezwa katika ubora na ufanisi unaoendana na thamani ya fedha iliyotolea “, ameeleza Dkt. Mollel.

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: +255 621 896 990

Pages