Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA), Ndugu Kiula Kingu amekagua maendeleo ya ujenzi wa jengo la "Maji House" lililo katika hatua za mwisho za utekelezaji.
Mradi huu unatekelezwa na mkandarasi kampuni ya Civil Engineering Construction Corporation (CCECC) ambapo kwa sasa imefikia zaidi ya asilimia 95 ya utekelezaji.