Breaking

Sunday, 29 October 2023

UBIA WA BARRICK NA TWIGA WAPONGEZWA KWA KUENDELEA KULETA MAFANIKIO MAKUBWA KATIKA SEKTA YA MADINI NCHINI TANZANIA


Meneja wa Barrick nchini Melkiory Ngido,akieleza utendaji wa shughuli za kampuni ulivyofanikisha kuleta mabadiliko chanya wakati wa mkutano wa Jukwaa la kimataifa la uwekezaji katika sekta ya madini uliomalizika jijini Dar es Salaam.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na Waziri wa Madini,Antony Mavunde wakipata maelezo ya uendeshaji wa shughuli za kampuni ya Barrick nchini kwa kushirikiana na Twiga kutoka kwa Meneja wa Mawasiliano na Uhusiano wa Barrick,Georgia Mutagahywa wakati wa mkutano wa Jukwaa la kimataifa katika sekta ya madini unaoendelea uliomalizika jijini Dar es Salaam (kushoto) ni Makamu wa Rais wa Utafiti wa Madini wa Barrick Gold Corporation, Nathan Komarnisky.
Mshauri wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,William Lukuvi,akipata maelezo ya shughuli za Barrick kutoka kwa Meneja wa Fedha wa Barrick,Penina Kituku wakati akipotembelea banda la kampuni kwenye mkutano huo.
Wafanyakazi wa Barrick wakionyesha tuzo ambazo kampuni imejishindia wakati wa mkutano huo.
Baadhi ya wafanyakazi wa Barrick walioshiriki katika mkutano huo katika picha ya pamoja baada ya kumalizika mkutano.
Washiriki Mbalimbali walipata fursa ya kutembelea banda la Barrick kwenye mkutano huo.

***
Ubia wa Serikali ya Tanzania kupitia kampuni ya Twiga na kampuni ya Dhahabu ya Barrick umepongezwa na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa kwa jinsi unavyoendelea kufanikisha kuleta faida za kiuchumi na athari chanya za kimageuzi za uchimbaji madini nchini.

Waziri Mkuu alitoa pongezi hizo alipotembelea banda la maonesho la Barrick na Twiga, kwenye mkutano wa mkutano wa Jukwaa la kimataifa la uwekezaji katika sekta ya madini uliomalizika jijini Dar es Salaam ambao aliufunga rasmi “Nawapongeza kwa kazi nzuri mnayofanya katika kuchangia maendeleo ya wananchi kupitia sekta ya madini na kufanikisha miradi ya kijamii katika maeneo yanayozunguka migodi”alisema.

Viongozi wengine wa Serikali, Wabunge, wadau wa Sekta ya madini na Wananchi waliopata fursa ya kutembelea banda hilo la maonesho la Barrick na kupatiwa maelezo kuhusiana na utendaji wa kampuni wamepongeza jitihada za kampuni inazofanya nchini kutekeleza miradi endelevu ya kuboresha maisha ya wananchi pia kwa kuwa kinara wa kuchangia pato la taifa.

Awali akitoa wasilisho kuhusiana na utendaji wa Kampuni kwenye mkutano huo, Meneja wa Barrick Nchini, Melkiory Ngido, alibainisha kuwa ubia wa Barrick na Serikali uliyoiunda kampuni ya Twiga unahakikisha pande zote mbili zinagawana kwa usawa faida za kiuchumi zinazotokana na migodi ya North Mara na Bulyanhulu.

Pia imebainishwa kwamba tangu mwaka 2019 ilipoichukua migodi hiyo iliyokuwa imekufa, Barrick Imeibadilisha na kuifanya kuwa na viwango vya kimataifa, vilevile kampuni kipindi hicho kampuni imechangia zaidi ya dola bilioni 3 katika uchumi wa Tanzania ambapo mwaka huu Twiga ilitambuliwa kuwa mlipaji mkubwa kuliko makampuni yote ambayo Serikali ina maslahi nayo.

Migodi ya Barrick hutumia asilimia 84 ya bajeti yake ya manunuzi kwa makampuni ya ndani huku asilimia 96 ya nguvu kazi yake ikiwa ni ya wananchi wa Tanzania.

Kupitia sera ya Uwajibikaji Kwa jamii (CSR) kampuni imeishatuimia kiasi cha Dola za Kimarekani 13.2 kutekeleza miradi ya kijamii katika maeneo yanayozunguka migodi katika sekta mbalimbali ikiwemo kuboresha elimu, Afya, Miradi ya maji Safi, Na kuimarisha miundombinu ya barabara. Miradi hiyo imefanikisha kuleta ubora wa maisha katika jamii zinazozunguka migodi yake.

Mwaka huu Barrick pia imetoa dola milioni 40 kwenye mpango wa ujenzi wa barabara na dola milioni 30 zaidi katika uboreshaji wa suhula za elimu ya juu nchini.

Kampuni pia imekuwa mstari wa mbele kutekeleza kanuni za usalama kupitia mpango wake ujulikanao kama Journey to zero ambapo mwaka huu migodi yake imefanikiwa kunyakua tuzo kubwa za Afya na Usalama mahali pa kazi kutoka Mamlaka ya Tanzania Occupational Safety and Health Authority (OSHA).

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: +255 621 896 990

Pages