Breaking

Thursday, 12 October 2023

TVLA YATEMBELEA WADAU KUJUA CHANGAMOTO ZAO ILI KUBORESHA HUDUMA

Mmoja wa wauzaji wa bidhaa za Wakala ya Maabara ya Veterinari Tanzania-TVLA kutoka duka la Mashina Agrovet lililopo Morogoro, akifurahia kuletewa chanjo ya mdondo wa Kuku siku ya tarehe 11/10/2023 alipotembelewa dukani kwake na wataalam wa TVLA kwa lengo la kutangaziwa huduma zinazotolewa na TVLA, kusikilizwa maoni yao pamoja na kutatua changamoto wanazokutananazo kutoka kwa wateja wanaotumia bidhaa za TVLA. Aliesimama kulia ni Bw. Prosper Haule Kaimu Mkuu wa idara ya Mipango, Masoko na Habari na aliesimima kulia ni Bwa. Salim Mbalazi Mtaalam kutoka TVLA
Kaimu Mkuu wa Idara ya Mipango, Masoko na Habari kutoka Wakala Wakala ya Maabara ya Veterinari Tanzania (TVLA) Bw. Prosper Haule akikabidhi chanjo ya mdondo wa kuku aina ya TEMEVAC kwa Bi. Alice Tenga Muuzaji wa duka la pembejeo za Mifugo (Temboni VET) lililopo Goba jijini Dar es Salaam Oktoba 10, 2023 alipofanya ziara ya kutembelea maduka yanayouza bidhaa za TVLA kwa lengo la kutangaza huduma zinazotolewa na TVLA, kusikiliza maoni pamoja na kutatua changamoto wanazokutananazo kutoka kwa wateja wanaotumia bidhaa za TVLA.
Kaimu Mkuu wa Idara ya Mipango, Masoko na Habari kutoka Wakala Wakala ya Maabara ya Veterinari Tanzania (TVLA) Bw. Prosper Haule (katikati) akitoa elimu ya utambuzi wa chanjo zinazozalishwa na TVLA kwa Bi. Mariam Kalisyna Muuzaji wa duka la pembejeo za Mifugo (Kalisyna VET) lililopo Mwenge jijini Dar es Salaam Oktoba 10, 2023 alipofanya ziara ya kutembelea maduka yanayouza bidhaa za TVLA kwa lengo la kutangaza huduma zinazotolewa na TVLA, kusikiliza maoni pamoja na kutatua changamoto wanazokutananazo kutoka kwa wateja wanaotumia bidhaa za TVLA.
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: +255 621 896 990

Pages