Breaking

Saturday, 14 October 2023

TVLA YASHIRIKI MAEONESHO YA SABA YA KUKU NA NDEGE WAFUGWAO

Mtaalamu wa Maabara wa Wakala ya Maabara ya Veterinari Tanzania (TVLA) Bi. Christine Nsimba akitoa elimu kuhusiana na namna TVLA inavyofanya uhakiki wa ubora wa vyakula vya mifugo kwa kutumia mashine ya kisasa ya mionzi ya kupima viwango vya viini lishe (Near Infrared) kwa mdau wa ufugaji alietembelea banda la TVLA kwenye maeonesho ya saba ya Kuku na Ndege wafugwao yanayofanyika kwenye ukumbi wa Mlimani City, jijini Dar es Salaam kuanzia Oktoba 13 -14, 2023.
Mkuu wa kitengo cha Sayansi ya Wanyama wa Wakala ya Maabara ya Veterinari Tanzania (TVLA) Dkt Scholastica Doto (kulia) wakitoa maelezo kwa wadau wa mifugo waliotembelea banda la TVLA kuhusiana na matumizi sahihi ya Chanjo ya Mdondo/kideri (TEMEVAC), uhakiki wa ubora wa vyakula vya mifugo aina ya kuku pamoja na huduma mbalimbali zinazotolewa na Wakala kwenye maeonesho ya saba ya Kuku na Ndege Wafugwao yanayofanyika kwenye ukumbi wa Mlimani City, jijini Dar es Salaam kuanzia Oktoba 13 -14, 2023.
Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mipango, Masoko na Habari kutoka Wakala Wakala ya Maabara ya Veterinari Tanzania (TVLA) Bw. Prosper Haule akitoa elimu kwa mdau wa Mifugo alietembelea banda la TVLA kujifunza kazi zinazofanywa na TVLA pamoja matumizi sahihi ya chanjo za Mifugo zinazozalishwa na TVLA kwenye maeonesho ya saba ya Kuku na Ndege wafugwao yanayofanyika kwenye ukumbi wa Mlimani City, jijini Dar es Salaam kuanzia Oktoba 13 -14, 2023. Kushoto kwake ni Mtaalamu wa Maabara TVLA Bi. Christine Nsimba na Mkuu wa kitengo cha Sayansi ya Wanyama wa TVLA Dkt Scholastica Doto.
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: +255 621 896 990

Pages