Breaking

Saturday, 14 October 2023

TGNP YAADHIMISHA SIKU YA MTOTO WA KIKE DUNIANI KWA KUTOA MAFUNZO KWA KLABU ZA JINSIA

NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM

KLABU za Jinsia Shule za Msingi na Sekondari wamepewa mafunzo na Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) katika kusherehekea Siku ya Mtoto wa Kike Duniani yenye la kuimarisha mtoto wa kike kutambua haki zake, kujiamini na kuhakikisha anafikia ndoto zake.

Akizungumza Oct 14,2023 wakati wa mafunzo hayo Kaimu mkuu wa idara ujenzi wa nguvu za pamoja na harakati wa TGNP, Bi. Frola Ndaba amesema, taasisi yao imejikita katika kuhakikisha inampa kipaumbele mtoto wa kike,katika nyanja mbali mbali za maisha ili kumuinua na kumpa hali ya kuwa kiongozi kuanzia akiwa kijana.

"Tunapokua tunaadhimisha siku hii moja ya kipaumbele chetu ni kugusa moja kwa moja mambo yanayo mgusa mtoto wa kike, suala la elimu kwa wote hasa kwa masomo ya sayansi,Afya na ustawi"Amesema.

Aidha Bi. Frola amesema dira ya miaka 25 inafikia ukomo hivo wanafanya maandalizi kuwaandaa watoto wakue wakijua na kuelewa masuala yao ili waweze kusema hata wanapo andaa dira ya miaka mingine 25 ijayo ni Mambo gani wanatamani Serikali iyaweke kwa ajili yao.

"Tupo katika wakati tunaolekea katika uchaguzi, nijambo kubwa kuongea kuhusiana na masuala ya jinsia tusipoona wanawake wengi wakijitokeza tutajiuliza je!huko mashuleni na vyuoni Kuna watu wanaonitokeza"Amesema

Pamoja na hayo amesema lengo la mafunzo hayo ni kuibua hamasa na kujiamini na kupeana ujuzi kuhusiana na masuala mbali mbali hivyo kupitia Changamoto wanazo pitia watapata nguvu kupitia wengine ambao waliwahi kuya pitia na kushinda.

Mafunzo hayo yalikuwa na kauli mbiu isemayo WEKEZA KATIKA HAKI ZA WASICHANA, UONGOZI WETU,USTAWI WETU, ambapo kila ifikapo Oktoba 11 kila mwaka huadhimishwa Siku ya Mtoto wa Kike Duniani.
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: +255 621 896 990

Pages