Breaking

Wednesday, 25 October 2023

MIKOCHENI WAKUMBUSHWA KULIPIA HUDUMA YA MAJI

Zoezi la uhamasishaji ulipaji wa bili za maji kwa watumiaji wa huduma za majisafi na usafi wa Mazingira ikiendelea katika mitaa ya Daima, Kifaru, Mwalimu Nyerere, Rose Garden, Ruvu na Manyara katika Kata ya Mikocheni A Wilaya ya Kinondoni.

Kazi hii imeambatana na utoaji wa elimu ya matumizi bora ya maji, utunzaji wa maji pamoja na ulinzi wa miundombinu ya majisafi.

Mamlaka inaendelea kuwasisitiza wateja kulipia huduma za maji kwa wakati pindi wanapopata bili zao ili kuiwezesha DAWASA kuboresha huduma.


Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: +255 621 896 990

Pages