Breaking

Tuesday, 3 October 2023

MHE.KIGAHE AZIAGIZA BRELA NA SIDO KUFIKA NGAZI ZA HALMASHAURI KUWAWEZESHA WAFANYABIASHARA

Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe Exhaud Kigahe (Mb.) ameziagiza BRELA, SIDO na Taasisi husika kufika katika Ngazi za Halmashauri ili kuwawezesha Wafanyabiashara.

Amesema hayo Octoba 3,2023 akiwa anafunga Kongamano la Biashara na Uwekezaji wilayani Pangani Jijini Tanga lililofanikiwa kuwakutanisha wafanyabishara mbalimbali mkoani Tanga.

Aidha, Kigahe amesema Serikali ya Awamu ya Sita inaendelea kuboresha mazingira ya biashara na uwekezaji na kuhakikisha sekta binafsi zinafanya vizuri katika maendeleo ya biashara na uchumi

Aidha amewataka wafanyabiashara, Wadau wa Maendeleo na Wajasiliamali kuchangamkia Fursa za utalii, kilimo, ufugaji na uchumi wa bluu katika wilaya ya Pangani

Vilevile, Kigahe amesema ni wakati sasa thamani ya Malighafi nchini iongezeke iwe maradufu na nchi iwe inazalisha bidhaa zilizokamilika ili ziweze kuingia katika Soko Huru la Biashara Afrika na Masoko mengine ndani na nje ya Afrika

Vilele amempongezaa Mkuu wa Wilaya ya Pangani Bi Zainab Issah kwa maandalizi ya Kongamano hiloo nakua Mkuu wa Wilaya wa Kwanza Nchini Kuaanda "Pangani Royal tour" itakayofungua milango katika Vivutio mbali mbali ikiwemo Hifadhi ya Saadani , Zao La Mwani, Uchumi wa Bluu, Kilimo na Ufugaji

Naye Mkuu wa Wilaya ya Pangani Mhe Zainab Issah ameishukuru Serikali ya Awamu ya Sita kwa kuifungulia maendeleo Pangani kwa ujenzi wa barabara Tanga-Pangani-Saadani-Bagamoyo, Daraja la mto Pangani na Miradi mbali mbali ya Maendeleo ili kuweza kuhamasisha uwekezaji na muingiliano wakibiashara ndani na nje ya nchi.



Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: +255 621 896 990

Pages