Na Chalila Kibuda, Michuzi TV
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tamisemi Mohamed Mchengerwa amesema kuwa DART ijiimarishe kutoa huduma ya usafiri katika jiji la Dar es Salaam kwa kuondoa malalamiko ya wananchi kuhusiana na usafiri huo.
Kujiimarisha katika kutoa huduma hiyo kwa miradi yote itapokamilika ndio itakwenda kuaksi utoaji wa huduma ya usafiri katika katika majiji mengine.
Mchengerwa amesema hayo wakati alipotembelea Wakala wa Mabasi Yaendayo Haraka (DART) kwa kukutana na menejimenti ya wakala huo jijini Dar es Salaam.
Mchengerwa amesema mradi wa mabasi hayo ni siasa kubwa ya kiuchumi kwa jiji la Dar es Salaam hivyo DART inatakiwa kushirikiana na mtoa huduma ya usafiri UDART.
Hata hivyo amesema kuwa kwa katika utoaji wa huduma ya usafiri kwa awamu zingine kunatakiwa kuwepo na ushindani kwa kuwa na kampuni zaidi ya mmoja ili kutoa huduma hiyo kwa ufanisi.
Aidha amesema kuwa Rais Dkt.Samia ameongeza furaha kwa wananchi hivyo watendaji ikiwemo DART kusimamia usafiri huo ili kuongeza furaha ya mtu kukaa muda mchache tu wakati akitaka kusafiri kutoka sehemu moja kwenda nyingine.
Mchengerwa ametaka watendaji kuacha kufanya kazi kwa mazoea na wataofanya hivyo ni mwepesi katika kuchukua maamuzi ambapo rekodi yake iko pale kwa kila sehemu aliyopita alifanya maamuzi dhidi ya watumishi ambao hawakutekeleza majukumu yao ipasavyo.
Mchengerwa amesema kuwa katika kufanya kazi ya usafirishaji kwa jiji la Dar es Salaam hataki kusikia malalamiko yanayotokana na usafiri wa mabasi yaendayo haraka.
Waziri huyo amesema kuwa katika masuala ya kufidia wananchi wafudiwe kwa wakati ili miradi iendelee kujengwa bila kuacha manunguniko.
Mchengerwa amesema kutengenezwe utaratibu kwa wanaotaka kupita kwenye miundombinu ya mabasi yaendayo haraka kulipia fedha hiyo ni moja ya kuongeza mapato
Amesema hakuna ubaya kwa watu kulipia kwenye barabara hizo kwani wanaonyesha kupenda mradi huo.
Kwa upande wa Mtendaji Mkuu wa DART Dkt.Edwin Mhede amemhakikishia Waziri kuendelea kutoa na kusimamia huduma bora ya usafiri katika jiji la Dar es Salaam.
Amesema kuwa katika miradi hiyo kuna ujenzi wa miundombinu kutoka Chanika hadi Mbagala kutokana na kuwepo kwa uhitaji mkubwa wa usafiri huo.
Dkt.Mhede amesema kuwa wanachukua hatua pale watakapoona kuna tatizo ya wanachukua hatua mara moja iwe kwa dereva au watoa huduma wengine.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tamisemi Mohamed Mchengerwa akizungumza na Menejimenti ya Wakala wa Mabasi Yaendayo Haraka (DART) wakati alipotembelea wakala huo jijini Dar es Salaam.
Mtendaji Mkuu wa DART Dkt.Edwin Mhede akitoa maelezo kuhusiana na utendaji wa DART wakati Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tamisemi Mohamed Mchengerwa wakati alipotembelea DART jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tamisemi Mohemed Mchengerwa akipata maelezo kutoka kwa Mtendaji Mkuu wa DART Dkt.Edwin Mhede wakati waziri huyo kwa mara ya kwanza kutumia usafiri wa mabasi yaendayo haraka katika jiji la Dar es Salaam.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tamisemi Mohemed Mchengerwa akizungumza katika kituo cha mabasi yaendayo Haraka Gerezani jijini Dar es Salaam.