Breaking

Saturday, 14 October 2023

MBUNGE DKT. MZAVA AKABIDHI MAJIKO YA GESI KWA MAMA LISHE KUHAMASISHA UTUNZAJI MAZINGIRA



Na Elias Gamaya Amo Blog Shinyanga

 KATIKA kuunga mkono jitihada za Rais wa Jamhuri wa muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan za kuhifadhi mazingira Mbunge wa viti maalumu mkoa wa Shinyanga Dkt. Christina Mzava amekabidhi majiko ya gesi kwa mama lishe wa kata ya  Itwangi Halmashauri ya Shinyanga kwani mama lishe ni watumiaji wakubwa wa nishati ya kuni hali inayotajwa kuchochea uharibifu wa mazingira katika maeneo hayo.

 Hafla ya kukabidhi majiko hayo imefanyika leo Oktoba 14,2023 katika kata ya Itwangi Halmashauri ya Shinyanga mkoani humo.

 Akikabidhi majiko hayo Dkt. Mzava amesema siku za hivi karibuni kumekuwa na mabadiliko ya tabia nchi hali inayochangiwa na ukataji wa miti ovyo unaofanywa na baadhi ya wananchi wakati wa kutafuta nishati ya kuni na mkaa kwa ajili ya kupikia .

 Dkt. Mzava ameeleza kuwa kupitia changamoto hiyo Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan amekuwa akisisitiza wawakilishi wa wananchi wakiwemo wabunge kutoa elimu juu ya athari za ukataji miti hovyo na uchomaji wa mkaa ikiwa ni sehemu ya kutekeleza Ilani ya Chama Cha Mapinduzi ya 2020-2025 kuhakikisha mazingira yanakuwa salama kwa kuepuka kukata miti hovyo.

 Pia Dkt. Mzava amesema kuwa mitungi hiyo iliyokabidhiwa ni kwa ajili ya mfano kuonyesha namna matumizi ya mitungi ya gesi inavyosaidia kutunza kuhifadhi na kutunza mazingira.

Katika hatua nyingine, Dkt. Mzava ameahidi kuchangia shilingi  500,000/= kwa ajili ya kumalizia ujenzi wa jengo la Zahanati ya kijiji cha Itwangi linalojengwa kwa nguvu za wananchi wa kijiji hicho.

 "Katika jengo hilo lilioanzishwa kwa nguvu za wananchi kwa lengo la kuokoa afya za akina mama wajawazito na watoto hususani wakati wa kujifungua hivyo mimi nitachangia shilingi 500,000/= laki tano ili kuongeza kasi ya umalizia jengo hilo ". Amesema Dkt. Mzava.

 Kwa upande wake Mwenyekiti wa Umoja wanawake wa chama cha mapinduzi UWT Mkoa wa Shinyanga Grace Samwely amewataka wananchi kudumisha umoja na mshikamano katika kukijenga Chama Cha Mapinduzi na kutekeleza ilani inayotekelezwa na chama hicho.

 "Hatuwezi kuendelea pasipo kuwa na upendo, na mshikamano ,nawaasa wananchi tushikamane pamoja kukitetea chama chetu na umoja wetu", amesema Grace. 

 Kwa upande wao baadhi ya Mamalishe waliopata majiko  hayo katika Kata ya Itwangi wamempongeza mbunge wa viti maalumu mkoa wa Shinyanga Dkt. Christina Mzava kwa kuwajali na kuwaptia majiko ya gesi kwani majiko hayo yanaenda kuleta chachu ya maendeleo ya familia zao , pamoja na kutunza mazingira kwa kutumia nishati ya Gesi.

 "Tunakushukuru sana Mhe. Mzava kwa kugusa maisha yetu sisi mama lishe ,tunakuahidi kwenda kuwa mabalozi wazuri wa kukemea uharibifu wa mazingira na kuhamasisha matumizi ya majiko ya gesi. 

Mbunge wa viti maalumu mkoa wa Shinyanga Dkt, Chirstina Mzava (katikati) akiwa na viongozi wa UWT Mkoa.
\
Mbunge wa viti maalumu mkoa wa Shinyanga Dkt, Chirstina Mzava (katikati) akiwa na viongozi wa UWT Mkoa .
Mbunge wa viti maalumu mkoa wa Shinyanga Dkt, Chirstina Mzava akiwa na viongozi wakifurahia mitungi ya gesi. 
 Mwenyekiti wa UWT mkoa wa Shinyanga,Grace Samwely akizungumza katika hafla ya ugawaji wa majiko kwa mama lishe Kata ya Itwangi.
Mjumbe balaza kuu Tifa UWT Christina Gule  akizungumza katika hafla ya ugawaji wa majiko kwa mama lishe.
Katibu wa UWT Halmashauri ya Shinyanga Magdalena Dodoma  akizungumza katika hafla ya ugawaji wa majiko kwa mama lishe.










Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: +255 621 896 990

Pages