Breaking

Sunday, 15 October 2023

MAYAI SIO ANASA; VIONGOZI DODOMA WAHAMASIKA, WACHANGIA MAYAI, SIKU YA YAI DUNIANI

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Bi Rosemary Senyamule, Mkuu wa Wilaya ya Dodoma, Mh. Jaffar Shekimweri na Katibu Wa Ccm Mkoa wa Dodoma Mh. Pili Augustine Mbanga ni miongoni mwa viongozi walioguswa na na kampeni ya SAB Investment, ya Changia Yai.

Katika kuadhimisha siku ya Yai Duniani, kampuni hiyo ya SAB Investment iliandaa kampeni ya Changia Yai kuhamasisha jamii kukumbuka umuhinu wa kula Mayai na kusaidia Kugawa Mayai kwa Watoto waishio kwenye vituo vyenye uhitaji.

Kampuni hiyo ambayo iliweka Kambi katika Maonesho ya Dodoma Ya Sasa Si Dodoma ya Zamani Yalifanyika katika Viwanja vya Mashujaa vya Zamani na ambayo yalikutana na siku hiyo ya Yai Duniani na kuwezesha wadau mbalimbali kujuika kuchangia Mayai kama sehemu ya kujitoa kwa jamii katika Kusherehekea Siku ya Yai Duniani. ambapo viongozi hao wa serikali nao waliguswa na kushiriki.

Mkurugenzi wa SAB investment Saida Bwanakheri walio endesha zoezi hilo wakati akiabidhi makasha yenye mayai kwenye vituo hivyo vya watoto yatima vilivyopo jijini Dodoma alisema siku hii imewasaidia Kukumbusha jamii kuwa mayai kwa watoto na watu wazima, ni Muhimu kwa Afya.

Naye Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Rosemary Senyamule, ambaye ni mmoja wa wachangiaji amesema siku hiyo ya Yai inaweza kutumika vyema katika kuleta Hamasa na elimu kwa kuondoka pia Imani potofu juu ya ulaji wa Mayai akisema kuna baadhi ya watu wanakataza wajawazito kula mayai wakidai kuwa watazaa watoto wenye vipara .. lakini si kweli. zoezi la uchangiaji Mayai liligusa wengi na hivyo kusaidia vituo kadhaa Mjini Dodoma kufurahia siku hiyo.

Naye Mkuu wa Wilaya Dodoma Mh. Jaffar Shekimweri amewapongeza kampuni ya SAB investment ambayo ilianzisha kampeni hiyo kwenye kusherehekea Siku ya yai Duniani kwa kuhamasisha jamii ulaji na uchangiaji Mayai kwa Watoto wenye uhitaji.

Siku ya Yai Duniani huadhimishwa kila Ijumaa ya pili ya mwezi Oktoba kila mwaka. Siku hii hutumika kuheshimu nguvu ya virutubisho hivi na kueneza faida zake ambapo mwaka huu imeangukia tarehe 13 ya October 2023. Mkurugenzi wa SAB Saida Bwanakheri alisema "Kampuni ya SAB inajishughulisha na miradi ya ufugaji kuku tumesherehekea siku hii kwa mara ya kwanza na kupeleka ujumbe kuwa mayai sio anasa bali protein ya Bei nafuu inayopaswa kuliwa na watu wote.."

Alisema "Tumefanya hivyo kwa kukumbusha jamii pia kuvifikia vituo ya watoto Wenye Uhitaji kwani watoto Hawa wanastahiki kula Mayai katika kujenga Afya zao,"

Zoezi Hilo la Ugawaji Mayai kwa vituo vya watoto wenye uhitaji lilienda sambamba na utoaji wa elimu kuhusu Faida za Mayai"

Wakati akipokea Mayai hayo Mkuu wa kituo Cha Alrahman Orphanage Center Kilichopo Changombe Dodoma.Bi Fatma Abdalllah alisema amefurahishwa kuona siku hii inaadhimishwa na kuipongeza kampuni ya SAB kwahamasa ya kuchangisha Mayai kwa Watoto wenye uhitaji kwani mwanzoni hawakuona umuhinu wa Mayai nakusema inapita hata mwaka watoto hawali Mayai kwani pia watu wengi hawakumbuki kuchangia Mayai lakini kwa kujifunza umuhinu wa Mayai sasa wanakwenda kuweka kwenye ratiba zao na wanaamini kilichofanywa na kampuni hiyo Sasa kinakwenda kuamsha watu kuona umuhinu wa Kuchangia Mayai kwenye vituo na hatimaye kuboresha Afya za watoto vituoni.

Saida Bwanakheri Mkurugenzi wa SAB investment alisema kupitia kampeni hiyo wameweza kuvifikia vituo vitatu vya Dodoma ambavyo ni Al Rahmaan orphanage center Kilichopo chang'ombe karibu na chinangali sec school, Asmaa Binti Shams Orphanage Center na New Hope orphanage Cha Children and women organization pia wanaamini jamii inaweza kuamka kupambana na udumavu kwani Mayai ni protein rahisi kuliko nyama.

"Pamoja na kua tumeanza hili litakua ni zoezi endelevu hasa katika kuhakikisha tunafikia Mikoa inayoongoza kwa udumavu kwa kutoa elimu ya nguvu ya Yai na hata kusapoti kaya masikini kupata protein hii muhimu."

"Tunawashukuru Sana washirika wetu wote waliojumuika nasi katika kampeni hii ya CHANGIA YAI. Mungu akawaongeze walipopunguza, Hakika ilikuwa faraja Sana kuona tabasamu la watoto Hawa wakila Mayai."
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: +255 621 896 990

Pages