Breaking

Tuesday, 31 October 2023

MADIWANI MANISPAA YA SHINYANGA WATAKA WAFANYABIASHARA WOTE WAENDE KWENYE MAENEO WALIYOPANGIWA

Mstahiki Meya wa Manispaa ya Shinyanga, Mhe. Elias Ramadhan Masumbuko akiongoza Mkutano wa Baraza la Madiwani wa Manispaa ya Shinyanga

Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog

Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga limeazimia Wafanyabiashara wote waende kwenye maeneo waliyopangiwa kufanyia biashara zao na si vinginevyo.

Azimio hilo limetolewa leo Jumanne Oktoba 31,2023 wakati wa Mkutano wa Baraza la Madiwani wa Manispaa ya Shinyanga uliofanyika katika ukumbi wa Halmashauri hiyo wa Lewis Kalinjuna.

Wakitoa hoja katika mkutano huo, Madiwani wametaka Wafanyabiashara waende kwenye maeneo waliyopangiwa badala ya kuendelea kufanya biashara kiholela na kukaidi maagizo wanayopewa mara kwa mara na Halmashauri kuwataka waende kwenye vizimba walivyopangiwa.


Akiongoza Mkutano huo, Mstahiki Meya wa Manispaa ya Shinyanga, Mhe. Elias Ramadhan Masumbuko amesema ni Biashara zote lazima ziende kwenye maeneo yaliyoelekezwa huku akimuagiza Mkurugenzi wa Manispaa ya Shinyanga Alexius Kagunze kuweka mkazo kuhusu suala hilo.


“Tuweke mkazo, wafanyabiashara wote hasa Nguzo nane, maelekezo yanatolewa kila mara, wanakaidi na kutoa faini, nikuombe mkurugenzi usimamie jambo hili kwa namna ya kipekee. Wafanyabiashara wa mbao na mirunda waelekee Chamaguha, Wafanyabiashara wa mitumba waende kwenye eneo la Ngokolo Mitumbani”,amesema Masumbuko.


“Haiwezekani wafanye biashara waendelee kuwa kwenye maeneo ambayo hayajaelekezwa. Tunataka biashara yoyote ambayo imeelekezwa ifike kwenye eneo husika waliloelekezwa na si vinginevyo, kama mfanyabiashara anapigwa faini na anarudi tena huyo hatufai”,ameongeza Masumbuko.


Katika hatua nyingine madiwani hao wakizungumzia kuhusu tahadhari ya uwepo wa mvua kubwa za El Nino, wameiomba Wakala ya Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) kuimarisha barabara pamoja na kuzibua ,mitaro,mito, makaravati na madaraja yaliyojiziba ikiwa ni sehemu ya kukabiliana na msimu wa mvua ili kuepuka madhara ya Mvua kubwa za El Nino, lakini pia TANESCO kuchukua hatua kwenye maeneo yenye changamoto ya miundombinu ili kuepuka madhara yanayoweza kujitokeza kipindi cha mvua.

Akitoa salamu wakati wa kikao hicho, Katibu wa CCM Wilaya ya Shinyanga Mjini Ally Majeshi amewashukuru na kuwapongeza waheshimiwa Madiwani na watendaji wa halmashauri kwa namna wanavyotumia vizuri fedha zinazotolewa na serikali kwa ajili ya miradi ya maendeleo.
Mstahiki Meya wa Manispaa ya Shinyanga, Mhe. Elias Ramadhan Masumbuko akiongoza Mkutano wa Baraza la Madiwani wa Manispaa ya Shinyanga leo Jumanne Oktoba 31,2023 - Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Mstahiki Meya wa Manispaa ya Shinyanga, Mhe. Elias Ramadhan Masumbuko akiongoza Mkutano wa Baraza la Madiwani wa Manispaa ya Shinyanga
Mkurugenzi wa Manispaa ya Shinyanga Alexius Kagunze akizungumza kwenye Mkutano wa Baraza la Madiwani wa Manispaa ya Shinyanga
Mkurugenzi wa Manispaa ya Shinyanga Alexius Kagunze akisoma taarifa kwenye Mkutano wa Baraza la Madiwani wa Manispaa ya Shinyanga


Naibu Meya wa Manispaa ya Shinyanga, Mhe. Zamda Shaban akizungumza kwenye Mkutano wa Baraza la Madiwani wa Manispaa ya Shinyanga

Naibu Meya wa Manispaa ya Shinyanga, Mhe. Zamda Shaban akizungumza kwenye Mkutano wa Baraza la Madiwani wa Manispaa ya Shinyanga
Mkurugenzi wa Manispaa ya Shinyanga Alexius Kagunze (kulia) akiteta jambo na Mstahiki Meya wa Manispaa ya Shinyanga, Mhe. Elias Ramadhan Masumbuko kwenye Mkutano wa Baraza la Madiwani wa Manispaa ya Shinyanga
Mkutano wa Baraza la Madiwani wa Manispaa ya Shinyanga ukiendelea
Mkutano wa Baraza la Madiwani wa Manispaa ya Shinyanga ukiendelea
Katibu wa CCM Wilaya ya Shinyanga Mjini Ally Majeshi akitoa salamu wakati wa mkutano huo


Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: +255 621 896 990

Pages