Breaking

Sunday, 8 October 2023

Maagizo ya Katibu Mkuu wa CCM yatekelezwa na Wizara ya Maji kufika eneo la mradi wa Katambike Kata Ugalla Wilaya ya Mpanda Mkoani Katavi

Leo mapema ( 08 Oktoba, 2023) Naibu Waziri wa Maji Mheshimiwa Mhandisi Maryprisca Mahundi amefika kwenye kata ya Ugalla iliyopo Wilayani ya Mpanda Mkoani Katavi kwa ajili ya kukagua mradi wa maji wa Katambike ikiwa ni utekelezaji wa agizo la Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Ndugu Daniel Godfrey Chongolo.

Baada ya kutembelea na kukagua utekelezaji wa mradi huo, Mheshimiwa Mahundi ametoa maelekezo kwa Mkandarasi anayetekeleza kuwa afanye kazi usiku na mchana kuhakikisha anakamilisha ujenzi wa mradi kabla ya tarehe 30 Oktoba, 2023 ili wananchi waweze kupata huduma ya majisafi na Salama.

Ameongeza kuwa endapo Mkandarasi huyo atashindwa kukamilisha ujenzi wa mradi kwa muda uliopangwa, Wizara itaendelea na utekelezaji wa kazi zilizobaki kwa kutumia utaratibu wa Force Account

Aidha, Mhe.Mahundi amesema atarudi tena wiki ya kwanza ya mwezi Novemba, 2023 kwa ajili ya kufuatilia utekelezaji wa mradi huo.

Naye, Mkuu wa Wilaya ya Mpanda Mheshimiwa Jamila Kimaro amesema kuwa atasimamia na kufuatilia mradi huo na kutoa mrejesho Wizara ya Maji kuhusu utekelezaji.

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: +255 621 896 990

Pages