Breaking

Thursday, 26 October 2023

DK. BITEKO ATEMBELEA BANDA LA BARRICK KWENYE MKUTANO WA JUKWAA LA KIMATAIFA LA UWEKEZAJI KATIKA SEKTA YA MADINI

Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto Biteko akisalimiana na Makamu wa Rais wa Utafiti wa madini wa Barrick kanda ya Afrika na Mashariki ya Kati, Nathan Komarnisky, wakati alipotembelea banda la Barrick mkutano wa Jukwaa la kimataifa katika sekta ya madini (Kulia) ni Waziri wa Madini Mh. Anthony Mavunde
Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto Biteko, akipata maelezo ya utendaji wa kampuni ya Barrick kutoka kwa Makamu wa Rais wa wa Utafiti wa Madini wa Barrick kanda ya Afrika na Mashariki ya Kati , Nathan Komarnisky, wakati alipotembelea banda la Barrick kwenye mkutano wa Tanzania Mining Investment Forum Kulia ni Waziri wa Madini Anthony Mavunde.

Waziri wa Madini,Antony Mavunde, akisalimiana na Makamu wa Rais wa Utafiti wa Madini wa Barrick kanda ya Afrika na Mashariki ya Kati, Nathan Komarnisky, wakati alipotembelea banda la Barrick lililopo kwenye mkutano wa Jukwaa la kimataifa katika sekta ya madini
Meneja wa Barrick nchini, Melkiory Ngido, akieleza mafanikio yaliyopatikana kutokana na ubia wa Barrick na Twiga katika kukuza uchumi wa nchi na kuboresha maisha ya wananchi kwa wajumbe wa mkutano wa kimataifa wa sekta ya madini (Tanzania Mining Investment Forum)
Washiriki mbalimbali wamekuwa wakitembelea banda la maonesho la Barrick na Twiga.
Washiriki mbalimbali wamekuwa wakitembelea banda la maonesho la Barrick na Twiga.
Baadhi ya wafanyakazi wa Barrick wanaoshiriki katika mkutano huo.

***

Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto Biteko, ametembelea banda la maonesho la Kampuni ya Uchimbaji Madini ya Barrick inayoendesha shughuli zake nchini kwa Ubia na Serikali kupitia Kampuni ya Twiga katika mkutano wa Jukwaa la Kimataifa katika Sekta ya Madini (Tanzania Mining Investment Forum) unaoendelea jijini Dar es Salaam na kupata maelezo ya shughuli mbalimbali zinazofanywa na kampuni kupitia migodi yake iliyopo nchini ya Bulyanhulu, North Mara na Buzwagi, sambamba na mafanikio yaliyopatikana tangu Barrick ianze kuendesha migodi nchini.

Dk. Doto Biteko alikuwa mgeni rasmi katika ufunguzi wa mkutano huo akimwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dk.Samia Suluhu Hassan.


Meneja Mkuu wa Barrick nchini, Melkiory Ngido, alitoa wasilisho katika mkutano huo wa kimataifa na kubainisha mafanikio yaliyopatikana kutokana na ubia wa Barrick na Twiga nchini katika uchimbaji wa madini ambao umefanikisha kuleta mapinduzi mbalimbali yenye tija ikiwemo kutoa mchango katika pato la Taifa, kuongeza fursa za ajira kwa Watanzania, kutekeleza miradi ya huduma za kijamii kupitia sera ya CSR, kuboresha sekta ya elimu sambamba na kuinua maisha ya wazabuni wa kitanzania.
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: +255 621 896 990

Pages