Na Mwandishi Wetu
MAMLAKA ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya Kanda ya Kaskazini imeteketeza viroba vya bangi kavu 237 na mbegu za bangi zenye uzito wa kilogramu 310 iliyokuwa tayari kwa kupandwa.
Akizungumza katika zoezi la kuteketeza bangi hizo dampo la Kikatiti Wilayani Arumeru,mkoani Arusha , Mkuu wa Operesheni wa Mamlaka hiyo Kanda ya Kaskazini ,Innocent Masangula amesema bangi hizo zilikamatwa katika operesheni maalum.
Amesema mifuko hiyo iliyopo kwenye viroba hivyo imekamatwa kutokana na operesheni maalum iliyofanyika maeneo mbalimbali eneo husika linalolima bangi wakiongozwa na Mkuu wa Wilaya ya Arumeru,Emanuela Kaganda
"Operesheni bado itazidi kuendelea ikiwemo utoaji elimu juu ya ulimaji zao mbadala lakini hatulali tutaendelea kupambana na dawa haya"
Ambapo DC Kaganda alisema bangi hizo zimeteketezwa eneo hilo na katika kipindi cha Septemba gunia 90 za bangi zilikamatwa Oktoba mwaka huu, gunia 225 na kupelekea jumla kuwa gunia 316 sanjari na kilo 310 za bangi.
"Gunia nyingine tumeziteketezwa shambani nyingine zimeteketezwa hapa,na tutaendelea na zoezi hili"
Ameongeza kuwa serikali imejipanga kutoa elimu juu ya dawa ya kulevya ikiwemo ulimaji wa zao mbadala ili waachane na madawa hayo.