Breaking

Wednesday 4 October 2023

DAWASA YATEMBELEA WATEJA TEMEKE, YABEBA MAONI, CHANGAMOTO




Katika kuboresha huduma kwa wateja wake msimu huu wa wiki ya huduma kwa wateja, Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) kupitia mkoa wa kihuduma DAWASA- Temeke imetembelea na kuzungumza na wateja wake kwa lengo la kusikiliza maoni na changamoto ili kuboresha huduma.

Sambamba na kuwatembela pia watumishi wa Mamlaka walitoa zawadi ikiwa ni sehemu ya kuthamini mchango wa wateja hao katika usimamizi mzuri wa huduma za DAWASA.






Afisa Huduma kwa Wateja DAWASA -Temeke, ndugu Eva Kessy amesema kupitia wiki ya huduma kwa wateja ni wakati wa kuthamini nafasi na mchango mzuri wa wateja katika kukuza na kuimarisha upatikanaji wa huduma.

Ndugu Mshindo Mlawa mmoja wa wateja waliotembelewa ameeleza kufurahishwa na namna DAWASA ilivyowakumbuka wateja wake na kuwaonesha thamani yao.

"Niwapongeze DAWASA kwa kufanya mageuzi makubwa kwenye utoaji wa huduma kwa ujumla, ni kazi kubwa imefanyika na sasa huduma imeimarika kwa kiasi kikubwa," amesema Ndugu Mlawa.

"Binafsi naridhishwa sana na huduma za DAWASA hata nikisafiri napata bili na naweza kulipa kwa wakati kwa njia ya simu bila usumbufu wowote, haya ni maboresho makubwa sana," amemalizia ndugu Mlawa.






Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: +255 621 896 990

Pages