Kazi ya matengenezo ya bomba kubwa la usambazaji maji la inchi 21 inaendelea kutekelezwa na mafundi wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es salaam (DAWASA) kwa lengo la kudhibiti upotevu wa maji katika eneo la Mkuki na Goldstar, Kata ya Gerezani.
Kukamilika kwa kazi hii kutarudisha huduma ya maji kwa wakazi wa maeneo ya Kinondoni, Ilala, City Center, Mikocheni, Upanga, Jangwani, Mchikichini na Keko ambao huduma ilikosekana tangu jana Oktoba 4,2023.
Kazi hii inategemewa kukamilika leo, Oktoba 5,2023.