Breaking

Thursday, 5 October 2023

CHONGOLO ANG'AKA KUSUASUA UJENZI BARABARA KIBAONI-STALIKE, ATOA MAAAGIZO KWA VIONGOZI

Na Mwandishi Wetu, Mlele

KATIBU Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi(CCM) Daniel Chongolo ameuagiza uongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mlele, TANROADS , Kampuni ya ushauri na Mkandarasi kukutana ili kuweka mikakati itakayosaidia kuongeza kasi ya ujenzi wa barabara ya Kibaoni - Stalike inayojengwa kwa kiwango cha lami.

Chongolo ametoa maagizo hayo leo baada ya kuona ujenzi wa barabara hiyo umekuwa wa kusuasua na hivyo kuutaka uongozi wa Wilaya hiyo ukiongozwa na Mkuu wa Wilaya Mlle Majid Mwanga kuhakikisha wanatafuta ufumbuzi utakaowezesha kasi ya ujenzi wa barabara hiyo kuongezeka.

"Wakati wa kuhitimisha ziara yangu Oktoba 7, 2023, nitamuita Waziri wa Ujenzi, Innocent Bashungwa aje kukagua maendeleo ya ujenzi wa barabara hiyo na kuwaeleza wananchi ni namna gani barabara hiyo itakamilishwa kwa spidi."

Kwa mujibu wa mradi wa ujenzi wa barabara hiyo yenye urefu wa zaidi ya Km 50 inayogharimu zaidi sh. Bil. 80, inajengwa na Kampuni ya China ya CRSG.

Awali akitoa taarifa kwa Chongolo, Kaimu Meneja wa TANROADS Mkoa wa Katavi, Albert Laizer amesema ujenzi wa kuwa umefika asilimia 11.2 nyuma ya utekelezaji ambao ulipaswa uwe asilimia 21.

Amefafanua mud umefika miezi 15 kati ya 36 iliyopangwa na hadi sasa mkandarasi ameshalipwa kianzio zaidi ya sh. Bil. 12.

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: +255 621 896 990

Pages