Breaking

Wednesday, 11 October 2023

Benki ya NBC Yasafirisha Wafanyabiashara Kwenda China Kushiriki Maonesho Canton Fair

Dar es Salaam; Oktoba 10, 2023: Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) kupitia klabu yake ya biashara ijulikanayo kama NBC B-Club imeratibu safari ya wafanyabiashara 10 kutoka maeneo mbalimbali nchini kwenda nchini China ili kushiriki Maonyesho ya Uagizaji na Uuzaji wa bidhaa za China maarufu kama Canton Fair yanayotarajiwa kufanyika hivi karibuni huko Guangzhou, China.

Zaidi, hatua hiyo inatarajiwa kutoa fursa kwa wafanyabiashara hao kukutana na wazalishaji halisi wa bidhaa mbalimbali ili kujifunza teknolojia rahisi sambamba na kutafuta muunganiko mpya wa kibishara na masoko baina yao wenyewe pamoja na wafanyabiashara kutoka China.

Akizungumza wakati wa semina elekezi kwa wafanyabiashara hao kabla ya safari iliyofanyika jana jijini Dar es Salaam, Mkuu wa Kitengo cha Wajasiriamali wa NBC Bw Mussa Mwinyidaho alisema hatua hiyo ni sehemu ya utekelezaji wa mipango ya klabu ya biashara ya benki hiyo wa kuwaunganisha wanachama wa klabu hiyo na fursa mbalimbali za kibiashara ndani na nje ya nchi.

“Huu ni mwendelezo tu wa mpango huu kwa kuwa tumeshandaa safari za namna hii kwa miaka kadhaa ila tulisimama kwa miaka michache hii kutokana na janga la Corona na sasa tupo tayari kuendelea na hatua yetu ya kwanza ya muendelezo huu ni Maonesho ya Canton nchini China’’

“Ni matumaini yetu kwamba wakiwa nchini China wafanyabiashara hawa ambao miongoni mwao wapo watoa huduma, wazalishaji na wauzaji wa bidhaa mbalimbali watajifunza mambo mengi ikiwemo teknolojia rahisi na mpya, wataongeza muunganiko wao kibishara na kimasoko hususani kimataifa pia watajifunza mbinu mbalimbali za kibiashara zitakazowasaidia kuboresha biashara zao,’’ alibainisha.

Kwa mujibu wa Bw Mwinyidaho, wakiwa njiani kuelekea China, wafanyabiashara hao watapata fursa ya kutembelea nchi ya Misri kwa muda mfupi kabla ya kuendelea na safari hiyo ambapo inatarajiwa watakaa nchini China kwa siku takribani 10 na watapata fursa ya kutembelea miji na maeneo mbalimbali kabla ya kurejea nchini Oktoba 22 mwaka huu.

Wakizungumza mara baada ya kupatiwa semina hiyo iliyoendeshwa na kampuni ya TBMC ambayo ndiyo itawaongoza wafanyabiashara hao katika safari hiyo, baadhi ya wafanyabiashara pamoja na kuishukuru benki ya NBC kwa mpango huo walisema wamejipanga kuitumia vema safari hiyo kwa kuhakikisha kwamba wanaenda kujifunza teknolojia mpya, kukutana na kujenga uhusiano na wazalishaji wa bidhaa mbalimbali zinazozalishwa nchini China pamoja na kutumia fursa hiyo kufanya manunuzi ya bidhaa mbalimbali.
“Binafsi nafanya biashara ya uagizaji na usambazaji wa kemikali za migodini hivyo naamini kupitia safari hii ninakwenda kufungua milango na fursa mpya ya kujionea teknolojia mpya na kemikali wanazotumia wenzetu katika shughuli zao za uchimbaji madini. Naamini kwa kuwa wenzetu wametutangulia kwenye shughuli hizi basi watakuwa na kemikali bora zaidi zitakazotusaidia huku kwetu…nawashukuru sana NBC kwa fursa hii,’’ alisema Bw Saimon Makoye mfanyabiashara kutoka Kahama, Shinyanga.
Mkuu wa Kitengo cha Wajasiriamali wa NBC Bw Mussa Mwinyidaho (katikati) akionyesha tiketi pamoja hati kusafiria sambamba na baadhi ya wafanyabiashara kutoka maeneo mbalimbali nchini ambao wanakwenda nchini China ili kushiriki Maonyesho ya Uagizaji na Uuzaji wa bidhaa za China maarufu kama Canton Fair yanayotarajiwa kufanyika hivi karibuni huko Guangzhou, China. Safari hiyo imeratibiwa na benki ya NBC kupitia klabu yake ya biashara ijulikanayo kama NBC B-Club. Hafla ya kuwaaga wafanyabiashara ilifanyika jana jijini Dar es Salaam.
Meneja Bidhaa na Huduma za Kibenki kutoka Benki ya NBC, Jonathan Bitababaje (aliesimama) akizungumza na wafanyabiashara ambao wanakwenda nchini China ili kushiriki Maonyesho ya Uagizaji na Uuzaji wa bidhaa za China maarufu kama Canton Fair yanayotarajiwa kufanyika hivi karibuni huko Guangzhou, China. Safari hiyo imeratibiwa na benki ya NBC kupitia klabu yake ya biashara ijulikanayo kama NBC B-Club. Hafla ya kuwaaga wafanyabiashara ilifanyika jana jijini Dar es Salaam.
Mratibu wa safari hiyo kutoka kampuni ya TBMC Bi Sarah Mauki akizungumza na wafanyabiashara ambao wanakwenda nchini China ili kushiriki Maonyesho ya Uagizaji na Uuzaji wa bidhaa za China maarufu kama Canton Fair yanayotarajiwa kufanyika hivi karibuni huko Guangzhou, China. Safari hiyo imeratibiwa na benki ya NBC kupitia klabu yake ya biashara ijulikanayo kama NBC B-Club. Hafla ya kuwaaga wafanyabiashara ilifanyika jana jijini Dar es Salaam
Mkuu wa Kitengo cha Wajasiriamali wa NBC Bw Mussa Mwinyidaho (katikati) akimkabidhi tiketi pamoja hati kusafiria Meneja Bidhaa na Huduma za Kibenki kutoka benki hiyo Jonathan Bitababaje ambae ataambatana wafanyabiashara ambao wanakwenda nchini China ili kushiriki Maonyesho ya Uagizaji na Uuzaji wa bidhaa za China maarufu kama Canton Fair yanayotarajiwa kufanyika hivi karibuni huko Guangzhou, China. Safari hiyo imeratibiwa na benki ya NBC kupitia klabu yake ya biashara ijulikanayo kama NBC B-Club. Hafla ya kuwaaga wafanyabiashara ilifanyika jana jijini Dar es Salaam.

Mkuu wa Kitengo cha Wajasiriamali wa NBC Bw Mussa Mwinyidaho (katikati) akiwakabidhi tiketi pamoja hati kusafiria baadhi wafanyabiashara ambao wanakwenda nchini China ili kushiriki Maonyesho ya Uagizaji na Uuzaji wa bidhaa za China maarufu kama Canton Fair yanayotarajiwa kufanyika hivi karibuni huko Guangzhou, China. Safari hiyo imeratibiwa na benki ya NBC kupitia klabu yake ya biashara ijulikanayo kama NBC B-Club. Hafla ya kuwaaga wafanyabiashara ilifanyika jana jijini Dar es Salaam.

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: +255 621 896 990

Pages