NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM
UMRI wa Mtanzania kuishi umeendelea kuongezeka ambapo katika Sensa ya Mwaka 1978 umri wa Mtanzania kuishi ulikuwa miaka 45 wakati wa sensa ya mwaka 2022 umri wa Mtanzania kuishi umefika miaka 65.
Mtakwimu Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu Dkt.Albina Chuwa, amesema hayo Dar es Salaam, wakati akifunga mkutano wa kuwajengea wakuu wa mikoa uwezo wa kuzitumia takwimu za Sensa.
Akizungumza katika mkutano maalum uliohusisha pia Wakuu wa Mikoa kwenye Ukumbi wa Diamond Jubilee, leo Agosti 31, 2023, Mtakwimu Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu Dkt.Albina Chuwa, amesema mchakato wa Sensa uliopita umekuwa na mafanikio makubwa na haijawahi kutokea kuwa na ushirikiano wa juu kama uliioneshwa na watendaji.
“Watanzania wanaendelea kuishi zaidi kwa kuwa na wastani wa miaka 69 wakati kwa Wanaume ni wastani wa miaka 62. Wanawake wanaishi miaka mingi zaidi kutokana na sababu kadhaa ikiwemo za kibaiolojia.” Amesema
Ameongeza kuwa Nchi nyingi zinakuja Tanzania kujifunza juu ya mchakato wa Sensa ulivyofanyika.
Pamoja na hayo amesema kuwa kiwango cha elimu kimeongezeka, watu wanaojua kusoma na kuandika imefikia zaidi ya Asilimia 80, upande wa Bara ni zaidi ya Asilimia 90.
Naye, Kamisaa wa Sensa ya Watu na Makazi, Mhe.Anne Makinda akizungumza katika mkutano huo amesema “Awamu ya kwanza ilikuw akufanya uchechemuzi, ya pili kuhesabiwa na ya tatu ni kupeleka elimu ya matokeo ya Sensa kwa wahusika.
Mtakwimu Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu Dkt.Albina Chuwa akisisitiza jambo wakati akizungumza katika mkutano maalum uliohusisha pia Wakuu wa Mikoa kwenye Ukumbi wa Diamond Jubilee, Agosti 31, 2023 Jijini Dar es Salaam
Mtakwimu Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu Dkt.Albina Chuwa akizungumza katika mkutano maalum uliohusisha pia Wakuu wa Mikoa kwenye Ukumbi wa Diamond Jubilee, Agosti 31, 2023 Jijini Dar es Salaam
Kamisaa wa Sensa ya Watu na Makazi, Mhe.Anne Makinda akizungumza katika mkutano maalum uliohusisha pia Wakuu wa Mikoa kwenye Ukumbi wa Diamond Jubilee, Agosti 31, 2023 Jijini Dar es Salaam