Breaking

Friday, 15 September 2023

WANAFUNZI WA VIPIMO NA VIWANGO CBE WAULA

Na Mwandishi Wetu

CHUO cha Elimu ya Biashara (CBE), kimefanya uwekezaji mkubwa wa vifaa vya kisasa kwenye idara yake ya vipimo na viwango hususan kwenye upimaji wa mafuta ya vyombo vya moto.

Hayo yalisemwa jana chuon hapo na Mkuu wa chuo hicho, Profesa Tandi Lwoga, wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu maboresho yanayofanywa na chuo hicho.

Alisema katika siku za hivi karibuni, CBE imekuwa kwenye safari ya maboresho makubwa ya maabara zake, ikichochewa na dhamira yake ya kutoa elimu bora zaidi kivitendo kwa wanafunzi wa chuo hicho.

“Nafurahi kushiriki nanyinyi habari za uwekezaji mkubwa ambao bila shaka utaboresha utoaji wetu wa elimu katika fani hii ya vipimo na viwango hasa katika eneo la upimaji wa mafuta ya vyombo vya moto (Dizeli, petroli, mafuta ya ndege), pamoja na Mafuta ya taa kwa kampasi zetu za Dar es Salaam na Dodoma,” alisema.

Aidha, Profesa Lwoga alisema mnyororo mzima wa uuzaji wa mafuta una jukumu muhimu katika uchumi wa nchi na ni uwanja unaoendelea kubadilika mara kwa mara.

“Ni muhimu kwamba wanafunzi wetu wa viwango na vipimo wapokee mafunzo ya kisasa na ya kina ili kufaulu katika sekta hii kwa kuzingatia lengo hili, chuo kimefanya uwekezaji mkubwa katika vifaa vipya vya kozi zetu za pampu ya mafuta,” alisema.

Profesa Lwoga alisema vifaa hivyo vinajumuisha mfumo mzima wa pampu za mafuta, utakaoundwa kwa mfano wa kituo cha mafuta kwa kuweka matenki ya ardhini ya kuhifadhia mafuta.

Alisema pia wataweka pampu za mafuta zenye mikono minne, mfumo wa kupima ujazo moja kwa moja na vifaa vya uhakiki wa upimaji wa ujazo katika vituo vya mafuta.

Akizungumzia umuhimu wa mfumo huo katika jamii, Profesa Lwoga alisema maabara hizo zitatumika kama maeneo ya kujifunza ambapo wanafunzi wa CBE wanaweza kupata uzoefu wa vitendo na kukuza ujuzi muhimu unaohitajika katika tasnia.

Alisema maabara hizo zitatoa fursa kwa wanafunzi wa kozi fupifupi mfano wauzaji wa mafuta na mafundi pampu kupata eneo sahihi la kujifunzia kivitendo.

Alisema maabara hizo zitasaidia kukuza utaalam vipimo nchini na nchi za ukanda wa Afrika mashariki na kati na hivyo kuendelea kuchagiza ubora katika mnyororo/ufuatiliaji wa vipimo ili kuhakikisha mlaji anapata anachostahili.

“Lakini na muuzaji anapata anachostahili kama wenzetu TBS wanavyosimamia viwango hivyo na Wakala wa vipimo wanavyosimamia utekelezaji wa sheria ya vipimo,” alisema.

Alisema maabara hizo zitasaidia kullisha soko la ajira (viwanda vya uzalishaji na uchakataji) zao lililo bora zaidi katika tasni ya viwango na vipimo na kusaidia kutoa ushauri wa kitaalam kivitendo unaoendana na mahitaji ya soko katika mnyororo ya upimaji na uuzaji wa mafuta.

Profesa Lwoga alisema zitasaidia pia kutoa mafunzo mtambuka ya kitaalam na kivitendo kwa jamii katika mashaka yao juu ya uuzwaji wa mafuta

“Tunatarajia kupokea vifaa vingine vitakavyojumuisha upimaji wa mita za maji na matenki ya mafuta. Hivyo Ninawahimiza wanafunzi wote kutumia vyema rasilimali hizi, kujitahidi kupata matokeo bora, na kutekeleza ndoto zao katika uwanja wa teknolojia ya vipimo inayokua kwa kasi sana hivi sasa.





Mkuu wa Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE), Profesa Tandi Lwoga, akizungungumza na waandishi wa habari kuhusu vifaa vipya vya idara ya vipimo na metrolojia vya vilivyonunuliwa na chuo hichon kwaajili ya maboresho ya ufundishaji chuoni hapo
Mkuu wa Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE), Profesa Tandi Lwoga, akimkabidhi kompyuta mmoja wa walimu wa chuo hicho ziliozonunuliwa kwaajili ya kuboresha ufundishaji chuoni hapo

Mkuu wa Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE), Profesa Tandi Lwoga, akimkabidhi kompyuta mmoja wa walimu wa chuo hicho ziliozonunuliwa kwaajili ya kuboresha ufundishaji chuoni hapo


Mkuu wa Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE), Profesa Tandi Lwoga, akimkabidhi kompyuta mmoja wa walimu wa chuo hicho ziliozonunuliwa kwaajili ya kuboresha ufundishaji chuoni hapo

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: +255 621 896 990

Pages