Breaking

Sunday, 3 September 2023

WANAFUNZI EAST AFRICA DODOMA WATIA FORA KWA VIPAJI

Na Mwandishi Wetu, Dodoma

KATIKA kukimarisha afya ya akili na mwili kwa wanafunzi shule ya Awali na Msingi ya East Africa iliyoko Kikuyu jijini Dodoma, imeanzisha somo la mchezo wa karate.

Mwalimu mkuu wa shule hiyo Evarist Runiba, alisema hayo jana wakati akizungumza kwenye mahafali ya kwanza ya darasa la saba ya shule hiyo.

Alisema michezo hiyo ni sehemu ya kuwasaidia kuimarisha afya za wanafunzi wao ili kufanya vizuri katika masomo yao na shunguli mbalimbali za kila siku.

“Shule yetu pamoja na kufundisha masomo mengine lakini pia tunafundisha lunga ya kichina na kifaransa lakin pia tunalo darasa la mchezo wa karate ambalo wanafnzi wote wanapata mafunzo wakiwa hapa shule”alisema

Alisema katika amchezo huo wa karate wanao walimu waliobobea katika mchezo huo hali ambayo itasaidia wanafunzi hao kuwa timamu kimwili na kiakili ili kuendelea kufanya vizuri katika masomo yao.

Mgeni rasmi Katibu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) mkoa wa Dodoma Pilly Mbaga, alisema amefurahishwa na vipaji mbalimbali alivyoona kwenye shule hiyo.

Alisema ni vyema shule zingine ziige mfano huo kwa kutenga muda mzuri wa wanafunzi kucheza na kuimba.

Aidha, alisema kuna wanafunzi wenye vipaji mbalimbali kama vilivyoonekana kwenye mahafali hayo na kwamba kama vipaji hivyo vikiendelezwa wanaweza kupatikana wasanii wakubwa nchini.

“Mnafanya vizuri sana na muendelee hivyo hivyo kwenye michezo na burudani kwasababu hawa wameonyesha vipaji vya aina yake natoa wito kwa shule zingine ziige,” alisema

Aidha, alisema michezo inawafanya wanafunzi wanakuwa na afya njema hali ambayo pia itachangia kufanya vizuri kwenye masomo na mitihani yao pia hivyo walimu wasione kama michezo ni kupoteza muda bila sababu.

“Mbalina masomo ya kawaida wapeni muda wa kucheza kuonyesha vipaji vyao, hawa lazima wapate muda wa kufanya mambo mengine yanayowapa furaha kama michezo,” alisema

Wanafunzi hao walionyesha umahiri mkubwa kwenye kuimba na kucheza nyimbo mbalimbali hali ambayo iliwafurahisha wageni na wazazi waliofika kwenye mahafali hayo ambapo wengine walikuwa wakiwatunza.
Wanafunzi wa shule ya East Africa iliyoko Kikuyu Dodoma wakionyesha umahiri wao wa michezo mbalimbali wakati wa mahafali ya shule ya awali na msingi yaliyofanyika mwishoni mwa wiki jijini Dodoma.

Mmoja wa wanafunzi wa shule ya East Africa iliyoko Kikuyu Dodoma akiigiza kama mtu mwenye kitambi wakati wa mahafali ya shule ya awali na msingi yaliyofanyika mwishoni mwa wiki jijini Dodoma.

Wanafunzi wa shule ya East Africa iliyoko Kikuyu Dodoma wakionyesha umahiri wao wa kucheza na kuimba nyimbo mbalimbali wakati wa mahafali ya shule ya awali na msingi yaliyofanyika mwishoni mwa wiki jijini Dodoma.

Wanafunzi wa shule ya East Africa iliyoko Kikuyu Dodoma wakionyesha umahiri wao wa michezo mbalimbali wakati wa mahafali ya shule ya awali na msingi yaliyofanyika mwishoni mwa wiki jijini Dodoma.

Wanafunzi wa shule ya East Africa iliyoko Kikuyu Dodoma wakionyesha umahiri wao wa kucheza mchezo wa Karate wakati wa mahafali ya shule ya awali na msingi yaliyofanyika mwishoni mwa wiki jijini Dodoma.

Wanafunzi wa shule ya East Africa iliyoko Kikuyu Dodoma wakionyesha umahiri wao wa kucheza na kuimba nyimbo mbalimbali wakati wa mahafali ya shule ya awali na msingi yaliyofanyika mwishoni mwa wiki jijini Dodoma.

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: +255 621 896 990

Pages