Breaking

Saturday, 23 September 2023

Wanafunzi Green Acres watia fora kwa vipaji

Na Mwandishi Wetu

WANAFUNZI wa Shule ya Msingi Green Acres, wamewapagawisha wazazi na wageni waalikwa kwenye mahafali yao baada ya kuzungumza kwa ufasaha lugha ya Kifaransa na Kichina.

Hayo yamejiri leo kwenye mahafali ya 23 ya shule hiyo Mbezi Beach Salasala, wakati wanafunzi hao wakionyesha maonyesho mbalimbali kwa wageni waalikwa na wazazi wao.

Wanafunzi hao wameonyesha umahiri huo kwa kuzungumza mambo mbalimbali kwa lugha hiyo kwa ufasaha huku wanafunzi wengine wakitafsiri kwa lugha ya kingereza hali iliyoibua shangwe.

Mmoja wa wazazi aliyefika kwenye mahafali hayo, Vick Minja ambaye mwanaye anahitimu darasa la saba aliwapongeza walimu wa shule hiyo kwa kujiongeza na kuamua kuwafundisha wanafunzi hao lugha za kichina na Kifaransa.

Alisema kwa dunia ya sasa mtu kuwa na uwezo wa kuzungumza lugha ya kingereza na kifarasa ni sifa ya ziara ya kupata kazi hivyo alisema kuna haja kwa shule zingine kuiga mfano kama huo.

“Wachina wanapatikana kote duniani na taifa lao linazidi kukua kiuchumi kwa hiyo mwanafunzi akijua kichina uwezekano wa kupata kazi ni mkubwa kwasababu wachina wanazidi kuja Afrika kuwekeza kwenye miradi mbalimbali,” alisema

Mkuu wa shule hiyo, Minani Kafugugu, alisema waliamua kuanza kuwafundisha wanafunzi wa shule hiyo lugha ya kichina baada ya kuona ni lugha ambayo inaendelea kuhitajika zaidi duniani.

Alisema kuna umuhimu kwa shule mbalimbali kufundisha lugha za kifaransa na kichina kwani mtu kufahamu lugha zaidi ya moja kunampa uhakika wa kupata ajira kulinganisha na wasiojua lugha hizo.

Alisema mbali na lugha hizo kitaaaluma shule hiyo iko vizuri na kwamba mwaka huu wanatarajia kupata matokeo makubwa kwenye mitihani ya darasa la saba.

Alisema wamekuwa wakipata matokeo makubwa kitaaluma kwenye mitihani ya kuanzia darasa la nne, la saba, kidato cha pili na cha nne na kwmba hayo yanatokana na kuajiri walimu wenye weledi , wanaojituma na wenye nidhamu ya kazi yao.

Wakati huo huo, wanafunzi wa shule hiyo walionyesha vipaji vya aina yake kwenye michezo mbalimbali waliyoonyesha kwenye mahafali hayo.

Wanafunzi hao walionyesha umahiri wa hali ya juu kwenye kucheza na kuimba nyimbo mbalimbali za bongo fleva hali iliyowaamsha wazazi kwenda kuwatunza kwa zawadi mbalimbali.

Mmoja wa wazazi, James Mloka alipongeza walimu wa shule hiyo kwa kuibua vipaji vya wanafunzi hao kwani kuna umuhimu wa wanafunzi kujifunza viytu zaidi mbali ya masomo ya darasani.

“Binafsi nimefurahi sana kuona wanafunzi wana vipaji vya aina hii nani muhimu shule zingine ziige kwa Green Acres kwasababu wanafunzi wanaweza kuwa na vipaji lakini visipoibuliwa wanaweza kubaki kama walivyo kwa hiyo kuwe na program ya kuibua vipaji kama ilivyo hapa,”alisema


Mkurugenzi wa shule za Green Acres, Jackline Rushaigo akizungumza wakati wa mahafali ya shule ya awali, shule ya msingi na kidato cha nne Green Acres Mbezi Beach Salasala katikati ni Naibu Mkuu wa Chuo cha Elimu ya Biashara CBE, Dk. Nasib Mramba ambaye alikuwa mgeni rasmi leo.
Mkuu wa shule hiyo, Minani Kafugugu, Mkurugenzi wa shule za Green Acres, Jackline Rushaigo na mgeni rasmi kutoka CBE, Dk. Nasib Rushaigo wakifuatilia mahafaali hayo ya 23

Wahitimu wa darasa la saba wa Green Acres wakifanya yao kwenye mahafali ya 23 ya shule hiyo ambayo yamefanyika leo maeneo ya shule hiyo, Mbezi Beach Salasala Dar es Salaam.

Wahitimu wa darasa la saba wa Green Acres wakiingia kwenye mahafali ya 23 ya shule hiyo ambayo yamefanyika leo maeneo ya shule hiyo, Mbezi Beach Salasala Dar es Salaam.

Wahitimu wa shule ya awali Green Acres wakifanya yao kwenye mahafali ya 23 ya shule hiyo ambayo yamefanyika leo maeneo ya shule hiyo, Mbezi Beach Salasala Dar es Salaam.




Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: +255 621 896 990

Pages