Breaking

Friday, 1 September 2023

WAHADHIRI VYUO VIKUU WATAKIWA KUKUTANA KUJADILI UFAULU WA WANAFUNZI

NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM

WADAU wa Elimu nchini wametakiwa kuweka mazingira wezeshi kwa wanafunzi kusoma masomo ya sayansi ili waje kusaidia uchumi wa nchi hapo baadae.

Hayo yamesemwa leo Agosti 31,2023 Jijini Dar es Salaam na Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne, Mhe.Dkt.. Jakaya Kikwete katika hafla kutambua mchango wa wadau katika sekta ya elimu.

Amesema wahadhiri wa vyuo vikuu wanatakiwa kukutana na kujadili changamoto zinazofanya wanafunzi kutokufanya vizuri katika masomo ya Sayansi hali ambayo itapelekea kukwama kwa baadhi ya shughuli katika nchi kwani vitu vingi vinahitaji Sayansi ili kuvikamilisha.

Aidha Dkt. Kikwete amesema kuwa utaratibu huo wa kukutana unatoa fursa nzuri kwa wadau kushirikiana na serikali kuendeleza sekta ya elimu nchini.

“Kutokana na hali hii tunapaswa kuandaa mkakati wa kujadili na kuelezea changamoto zinasababishwa wanafunzi wanafeli ili kuweka mikakati yetu sawa kazi ibaki kwa wanafunzi, ” amesema Dk. Kikwete.

Ameeleza kuwa Shirika la GPE limeanzishwa miaka 20 iliyopita likiwa na lengo la kusaidia elimu nchi zenye mapato ya chini, vita na mabadiliko ya Tabia nchi.

Amesema GPE inajihusisha na elimu kuanzia shule ya awali ,msingi na sekondari na kuhakikisha wanapata elimu na lazima iwe bora na usawa wa jinsia ukiwa umezingatiwa

Hata hivyo amasema zoezi la kuchangia katika sekta ya elimu ni kwa maslahi ya Taifa hivyo kitendo hiko kinawaleta watu waliochangia pamoja wadau wa elimu ndani na nje ya nchi.

Dk. Kikwete ni Mwenyekiti wa Bodi ya GPE yenye wajumbe 40 ambapo Desemba mwaka huu wanatarajia kufanya mkutano nchini Visiwani Zanzibar ikiwa ni mara ya kwanza mkutano huo kufanyika nchini tangu bodi hiyo ilipoundwa.

Kwa upande wake Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Profesa Adolf Mkenda amesema kazi kubwa hafla hiyo iliyoandaliwa na Wizara ya Elimu kwa kushirikiana na TAMISEMI na wadau mbalimbali ni kuchangia Sekta ya elimu ili kuifanya kuwa Bora zàidi na yenye tija Kwa maslahi ya nchi.

“Sera ya elimu na mafunzo mwaka 2014 tuliangalia mambo ya msingi ambayo yamewekwa hayajafanyiwa kazi ikiwemo elimu ya msingi itakuwa miaka sita na minne sekondari jumla 10 anamaliza shule akiwa na miaka 16,”amesema Profesa Mkenda.

Amesema sera ya mwaka 2014 wapo kwenye mchakato watapeleka ipitishwe bungeni na mapendekezo mwezi ujao yatapitishwa na baade kutangazwa.



Profesa Mkenda amesema lengo kubwa ni kuboresha elimu nchini na katika kuendeleza elimu kuna hitaji gharama wadau mbalimbali wakutane na kuendea kuchangia.






Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: +255 621 896 990

Pages