Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania- TPA imekabidhi vifaa Tiba vyenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 30 vikiwemoVitanda vya kujifungulia wakina mama ( Delivery Beds) 15 kwa Uongozi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mtwara -Ligula.
Vifaa hivyo vimekabidhiwa leo Septemba 9,2023 na Naibu Mkurugenzi Mkuu wa TPA Mhe. Juma Kijavara ambaye amemuwakilisha Mkurugenzi Mkuu wa TPA ambapo amemkabidhi Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Mhe. Kanali Ahmed Abbas ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Miaka 18 tangu kuanzishwa kwa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania - TPA.
“Mheshimiwa Mkuu wa Mkoa tunakuahidi sisi kama wana TPA tutaendelea kuunga mkono juhudi zako kama unavyotuunga mkono kwenye shughuli zetu za kila siku na tutakuwa bega kwa bega na wewe.” Amesema Mha. Kijavara
Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Mhe. Kanali Ahmed Abbas ameipongeza TPA kwa kurejesha kwa Jamii faida wanayopata na kutoa vifaa tiba hivyo kwa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mtwara- Ligula.
Aidha Mhe. Kanali Abbas ameipongeza Bandari ya Mtwara kwa kupiga hatua kubwa katika kuhudumia Shehena ya mzigo mbalimbali.
“ Bandari ya Mtwara imepiga hatua kubwa katika kuhudumia Shehena ambapo katika kipindi cha mwaka mmoja kuanzia 2022-2023 imehudumia Shehena zaidi ya Tani Milioni 1.6 na kuvuka lengo la Kuhudumia Shehena Tani Laki nne walilokuwa wamejiwekea.” Amesema Kanali Abbas