Breaking

Saturday, 30 September 2023

TIMU ZA MALIASILI NA UTALII ZAPONGEZWA KWA KUANZA VIZURI MASHINDANO YA SHIMIWI MKOANI IRINGA

 

Na Mwandishi Wetu, IRINGA

Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu wa  Wizara ya Maliasili na Utalii, Bw.  Bernard Marcelline ameipongeza timu ya wanawake ya Wizara hiyo kwa kuibuka mshindi kwenye mchezo wa kamba waliocheza dhidi ya Tume ya Sheria ETC.

Akizungumza leo kwenye Mashindano ya Shirikisho la Michezo ya Wizara na Idara za Serikali (SHIMIWI) yanayofanyika mkoani Iringa, Bw. Marcelline amesema kwa wale ambao walipoteza michezo mingine bado wanayo nafasi ya kujipanga zaidi ili hatimaye kupata ushindi. 

"Tuna imani kubwa mtafanya  vizuri zaidi na kwa niaba ya Menejimenti ya Wizara nimekuja kuwaambia kuwa wapo na ninyi katika kila hatua", amesema.

Aidha, amesema michezo hiyo ina malengo mbalimbali ikiwemo kujenga mahusiano ya kikazi kati ya taasisi zao na watu wanaocheza nao.

"Kwa hiyo ushindi wa kwanza ni kwamba mmeshiriki, Ushindi wa pili mnajenga mahusiano na taasisi nyingine", ameongeza.

Wakati huo huo, amesema Wizara inatambua juhudi hizo na  kujitolea kwao.

"Tunatambua kwamba mtapata vikombe.  Nitakuwa nanyi kesho wakati wa mechi nikiwatia moyo lengo letu hapa ni ushindi, Tushangilie vizuri, tuhakikishe hii kamba inakatika",amesema.
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: +255 621 896 990

Pages