Breaking

Wednesday, 27 September 2023

TGNP YATOA MAFUNZO YA KIJINSIA KWA KAMATI ZA ELIMU NA AFYA

NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM

MTANDAO wa Jinsia Tanzania (TGNP) wameendelea kutoa Mafunzo ya Siku tatu kwa Kamati za Afya na Elimu yenye lengo la kujenga uelewa wa dhana ya kijinsia katika kuzingatia kuingiza masuala ya jinsia katika Elimu na Afya.

Akizungumza wakati wa Mafunzo hayo Septemba 26,2023 Jijini Dar es Salaam, Mwezeshaji wa Semina hiyo, Bi. Mary Nsemwa amesema kuwa kama mtu hana uelewa dhana ya kijinsia katika kuzingatia kuingiza masuala ya kijinsia kwenye kupanga mipango ya maendeleo atapanga mipango atafanikisha lakini atakuwa kipofu wa kijinsia.

"Mfano kwenye Elimu suala la kijinsia kwenye kumwandikisha na kumtengenezea msichana mazingira wezeshi aweze kusoma vizuri kama mtoto wakike akiwa msafi apate sehemu ya kujisitiri anapokuwa katika hedhi ,kusipokua na mlengo wakijinsia shuleni inapelekea mtoto wakike kupoteza siku tatu hadi tano kila mwezi hapo Kuna kuwa hakuna usawa". Amesema

Aidha Bi.Nsemwa amesema katika kilimo haki na usawa katika umiliki wa rasilimali ardhi na uzalishaji wa mavuno yanayopatikana kuwe na haki ya maamuzi katika mgawanyo wa kile kinacho patikana kwenye uzalishaji.

"Mwanamke analima anazalisha lakini inapokuja kupeleka sokoni unakuta baba ametangulia pesa zinazo patikana baba kumpa mama ni utashi wake hata katika suala la pembejeo wanaume wengi ndio wanafaidi wanawake wengi hawana uwezo kupata nafasi katika kupata pembejeo za kilimo" Ameeleza

Kwa upande wake mmoja wa waliohudhuria mafunzo hayo,Michael Mbawe amesema wanawake wakiwezeshwa wanaweza kufanya Mambo makubwa na kuwa tegemeo katika nchi.

"Nina ahidi kuwa kioo kwa jamii nimejifunza kumbe wanawake ukiwasimamia vizuri wanaweza kufanya Mambo makubwa pia hata makundi mengine Kama walemavu sio kwamba hawawezi ukiwawezesha na kuwasimamia vizuri wanaweza kufanya Mambo makubwa". Amesema

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: +255 621 896 990

Pages