Breaking

Tuesday, 19 September 2023

TET YASHIRIKI KONGAMANO LA TATU LA KITAIFA LA HUDUMA ZA MAKTABA


Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya huduma za Maktaba Tanzania(BOHUMATA) Dkt.Mboni Ruzega akitia saini kwenye kitabu cha wageni mara baada ya kutembelea banda la Taasisi ya Elimu Tanzania(TET) katika Kongamano la tatu la Kitaifa la Huduma za Maktaba,Tamasha la Vitabu na Usomaji liloanza leo Septemba 19 hadi 21 katika viwanja vya chuo cha Benki Kuu Mwanza (BOT).

Taasisi ya Elimu Tanzania (TET) inashiriki pamoja na wachapishaji mbalimbali wa vitabu nchini.

Maonesho hayo ni muhimu kwani vitabu ni nyezo muhimu katika suala la ufudishaji na ujifunzaji .

Tamasha hilo linawakutanisha wachapishaji mbalimbali na wananchi wa kawaida ambao watapata nafasi ya kusoma vitabu mbalimbali vinaoneshwa kwenye maonesho hayo.

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: +255 621 896 990

Pages