Wajasiriamali nchini wameaswa kuzalisha bidhaa zenye ubora ili kuweza kuhimili ushindani katika soko la ndani na nje ya nchi
Haya yamesemwa na Bw. Issa Dadi, Afisa Udhibiti Ubora (TBS Kanda ya Mashariki) wakati akiwahudumia washishiriki wapitotembela banda la TBS katika maonesho ya Wajasiriamali wa halmashauri ya jiji la Dar es Salaam yaliyoandaliwa na iMBEJU CRDB yaliyofanyika viwanja vya mnazi mmoja.
Bw. Issa alitumia fursa hii kutoa elimu kuhusu masuala ya viwango, namna bora ya uzalishaji wa bidhaa kwa ukizingatia namna bora ya usafi lengo likiwa ni kuzalisha bidhaa bora na salama kwa watumiaji wa mwisho.
Pia alipata nafasi ya kuwaeleza namna wanavyoweza kupata alama ya ubora kwa kutumia huduma ya uthibishaji ubora wa bidhaa bila gharama yoyote kwa wajasiriamali kwani serikali kila mwaka hutengenga fedha ili wajasiriamali wadogo na wa kati wathibitishe ubora wa bidhaa zao ili waweze kufikia makoso makubwa ndani na nje ya nchi.
Kwa upande wake Afisa Masoko (TBS), Bi. Rhoda Mayugu amesema, TBS ilitumia maonesho hayo kuwaelimisha wananchi kuhusu faida na umuhimu wa kununua bidhaa zilizothibitishwa ubora wake pamoja na umuhimu wa kuangalia muda wa watumizi wa bidhaa husika kabla ya kununua bidhaa hizo kwani kwa kufanya hivyo hulinda usalama wa afya zao, na kuepuka hasara za kiuchumi zinazoweza kujitokeza
Pia TBS imewaasa wananchi kutokununua bidhaa hafifu na kutoa taarifa wanapokutana na bidhaa hafifu ama zile zilizozuiliwa kutumika ni hakika Tanzania haitokuwa na bidhaa hafifu na haitokuwa jalala la bidhaa hafifu. Aliongeza Bi. Mayugu