Breaking

Friday, 1 September 2023

RFB YATEMBELEA MIRADI YA UJENZI WA BARABARA ZANZIBAR

Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya Mfuko wa Barabara (RFB) Octavian Mshiu (aliyechuchumaa), akimsikiliza Mkandarasi kutoka Kampuni ya IRIS Abdelmalek Rahbaoul, inayotekeleza mradi wa ujenzi wa barabara za lami visiwani Zanzibar kwa kutumia teknolojia mbadala ya “chip seal” nzenye urefu wa km 275.9, wakati bodi hiyo ilipotembelea barabara ya Mchangani hadi Dongongwe (km 4.3) kujifunza teknolojia hiyo.

Abdelmalek Rahbaoul kutoka Kampuni ya IRIS Rahbaoul inayotekeleza mradi wa ujenzi wa barabara za lami kwa kutumia teknolojia mbadala ya “chip seal” visiwani Zanzibar zenye urefu wa km 275.9, akifafanua jambo kwa wajumbe wa Bodi ya Mfuko wa Barabara (RFB), wakati Bodi hiyo ilipotembelea barabara ya Mchangani hadi Dongongwe kujifunza teknolojia hiyo.

Wajumbe wa Bodi ya Mfuko wa Barabara (RFB), wakiwa kwenye picha ya pamoja na baadi ya wawakilishi kutoka Wakala wa Barabara Zanzibar, Mfuko wa Barabara Zanzibar pamoja na wawakilishi kutoka kampuni ya IRIS inayotekeleza mradi wa ujenzi wa barabara za lami kwa kutumia teknolojia mbadala ya “chip seal” visiwani Zanzibar, baada ya kukamilisha ziara ya kutembelea barabara za Mchangani hadi Dongongwe (km4.3) na Kibele hadi Cheju (km 4.1) kwa ajili ya kujifunza teknolojia hiyo.


Muonekano wa barabara ya Mchangani hadi Dogongwe (km 4.3) visiwani Zanzibar, iliyojengwa kwa kiwango cha lami na kampuni ya IRIS kwa kutumia teknolojia mbadala ya “chip seal” iliyotembelewa na wajumbe wa Bodi ya Mfuko wa barabara (RFB), mwishoni mwa wiki kujifunza teknolojia hiyo.Muonekano wa barabara ya Kibele hadi Cheju (km 4.1) visiwani Zanzibar, iliyojengwa kwa kiwango cha lami na kampuni ya IRIS kwa kutumia teknolojia mbadala ya “chip seal” iliyotembelewa na wajumbe wa Bodi ya Mfuko wa barabara (RFB), mwishoni mwa wiki kujifunza teknolojia hiyo.

Picha na Bodi ya Mfuko wa Barabara
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: +255 621 896 990

Pages