Tuesday, 19 September 2023

RAIS SAMIA AIPONGEZA TAASISI YA MAMA ONGEA NA MWANAO KWA KUSAIDIA JAMII

Na Mwandishi Wetu

RAIS Samia Suluhu Hassan ameipongeza Taasisi ya Mama Ongea na mwanao 2021 chini ya Mwenyekiti wake Steven Mengele maarufu Steve Nyerere kupitia kampeni yao ya SAMIA NIVISHE VIATU kwa namna inavyoisaidia jamii katika mambo mbalimbali.

Ametoa pongezi hizo leo Septemba 19, 2023 wakati akizungumza na wananchi kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika Viwanja vya Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Lindi.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa taasisi hiyo Stive Nyerere amesema kampeni ya SAMIA NIVISHE VIATU imeanza rasmi katika kijiji cha Namienje wilayani Luangwa kwa kuwavisha viatu 200 watoto wa Kijiji hicho.

Amesema Kampeni hiyo ndio imeanza Katika mkoa huo wa Lindi,lakini itakwenda katika Wilaya zake na baadae itahamia Mtwara na Ruvuma, lengo likiwa kufika mikoa yote nchini

Amesema taasisi yake imekuwa ikifanya shughuli mbalimbali za kijamii ikiwemo kampeni hiyo,lengo likiwa ni ' kusapoti' juhudi za Serikali na Rais Samia kwa ujumla.

"Kampeni hii tutalifanya nchi nzima tumelenga vijijini na tutalifanya wenyewe na si kukabidhi kwa uongozi wa shule kwani lengo letu kuhakikisha vinamfikia mlengwa" amesema Steve.

Aidha ameongezea kuwa Serikali ya awamu ya sita kwa kuweka miundombinu mizuri katika sekta ya elimu hivyo wanawajibu kama taasisi inayounga mkono juhudi zinazofanywa na Rais Samia kuhakikisha watoto wanaipenda shule.

Kampeni hiyo ilianza mwaka jana ambapo waligawa zàidi ya viatu 2000 kwa watoto katika mkoa ya pwani wilaya ya Kibiti na mkoa wa Tabora na wilaya zake.



Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: +255 621 896 990

Pages