Breaking

Friday, 15 September 2023

NAIBU WAZIRI WA MAJI MHANDISI MARYPRISCA ASHIRIKI MAADHIMISHO YA 12 YA MTO MARA.

Naibu Waziri wa Maji, Mhe.Mhandisi Maryprisca Mahundi kwa niaba ya Waziri wa Maji ameshiriki Maadhimisho ya 12 ya Siku ya Mto Mara, hafla hiyo imefanyika Mkoani Mara kwenye Viwanja vya Mugumu/Serengeti.

Wakati wa Hafla hiyo Mhe. Mahundi amesema kuwa Maadhimisho ya Bonde la Mto Mara ni njia muhimu ya kudumisha umoja wetu na ujirani mwema sisi wana Afrika Mashariki.

Muitikio huu ni dhahiri kuwa sisi ni ndugu wenye nia moja ya kuhifadhi na kusimamia vyema rasilimali za maji za Bonde la Mto Mara ambao ni kiunganishi cha umoja wetu, ustawi wa jamii na mataifa yetu; pamoja na mustakabali wa kizazi cha sasa na kizazi kijacho "amesema"

Aidha amesema kuwa Mto Mara unafaida nyingi sana ikiwemo Hifadhi ya Taifa ya Serengeti kwa upande wa Tanzania pamoja na pori la akiba la Hifadhi ya Taifa ya Maasai-Mara kwa upande wa Kenya ambapo Hifadhi hizi mbili ni kielelezo cha utalii duniani na uchumi wa mataifa yetu.

Hivyo, uhifadhi wake ni wa lazima na unadhihirisha maana ya maadhimisho ya siku ya Bonde la Mto Mara. Juhudi hizi ni uungaji wa dhamira njema ya Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika agenda yake ya kukuza utalii kupitia jitihada mbalimbali kama vile filamu ya The Royal Tour.

Naye, Mkuu wa Msafara kutoka Jamhuri ya Kenya Mheshimiwa Tamalinye Koech amesema kuwa Bonde la Mto Mara ni eneo muhimu kwa maendeleo ya kiuchumi kutokana na baionual zilizopo. Pia, ameendelea kusisitiza kuwa hizi Nchi mbili ( Tanzania na Kenya) ziendelee kutoa elimu juu ya umuhimu wa uhifadhi mazingira ya Bonde la Mto Mara.

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: +255 621 896 990

Pages