Breaking

Tuesday, 12 September 2023

MASHINDANO YA POLISI JAMII DPA CUP YAZINDULIWA RASMI

Na Abel Paul wa Jeshi la Polisi- Dar es salaam

Mashindano ya Polisi Jamii DPA Cup yamezinduliwa rasmi leo Septemba 12,2023 katika Viwanja vya chuo cha Taaluma ya Polisi Dar es salaam yakiwa yamebeba kauli mbiu isemayo Polisi jami kwa usalama na maendeleo yetu ambapo mgeni rasmi alikuwa Igridy Venancy Kimario afisa Michezo kutoka Manisapa ya Temeke akimwakilisha  Mkuu wa wilaya ya Temeke.

Akiongea katika ufunguzi wa michezo hiyo Igridy Venancy Kimario afisa Michezo kutoka Manisapa ya Temeke michezo amesema michezo inawaunganisha Jamii na kubadilishana Mawazo ikiwa ni Pamoja kupeana taarifa za wahalifu na uhalifu katika Jamii huku akilipongeza Jeshi la Polisi kwa namba ambavyo waendelea kuratibu mashindano ya Polisi Jamii na kueleta matokeo Chanya katika Jmaii.

Ameongeza kuwa licha ya michezo kuwa na faida kiuchumi amebainisha kuwa imeweza kubadilisha mitazamo hasi kwa vijana ambao wamekuwa ni wahathirika wakubwa katika kushawishika na makundi ya watu wabaya katika jamii wanazotoka.

Kwa upande wake Mkuu wa Chuo cha Taaluma ya Polisi Dar es salaam Kamishna msaidizi mwandamizi wa Polisi SACP Dkt. Lazaro Mambosasa amesema hapo awali kulikuwa na mitazamo hasi kwa Jeshi la Polisi ambapo amesema wao kama chuo walipokea maelekezo kutoka kwa Mkuu wa Jeshi la Polisi jinsi ya kuwafundisha kwa vitendo maafisa hao na wakaguzi wasaidizi wa Polisi dhana dhima ya ushirikishwa wa Jamii kwa vitendo ili pindi watakapo maliza mafunzo yao wakafanye kwa vitendo namna nzuri ya kushirikisha jamii katika  kutatua changamoto ya uhalifu hapa nchini.

Naye Afisa Michezo kutoka chuo cha Taaluma ya Polisi Dar es salaam Mrakibu mwandamizi wa Polisi SSP Salum Madongo amesema anamshukuru Mkuu wa chuo cha Taaluma ya Polisi Dar es salaam Kamishna msaidizi mwandamizi wa Polisi SACP Dkt. Lazaro Mambosasa kwa maelekezo mazuri ya uandaji wa michezo hiyo ambavyo matarajio yake ni kuwafundisha kwa vitendo namna bora ya kuwashikisha jamii katika kutatua changamoto ya uhalifu hapa Nchini.

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: +255 621 896 990

Pages