Breaking

Thursday, 7 September 2023

MAKATIBU NA WENYEVITI WA UWT KAHAMA WATUA BUNGENI DODOMA

Mbunge wa viti Maalum Mkoa wa Shinyanga, Mhe. Lucy Mayenga amewakabidhi Makatibu na Wenyeviti wa Umoja wa Wanawake CCM (UWT) wa Kata 112 kutoka wilaya ya Kahama shilingi milioni 11.2 kwa ajili ya  programu ya kuongeza Marafiki wa Chama Cha Mapinduzi sambamba na kuunga mkono jitihada zinazofanywa na  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia  Suluhu Hassan katika kuwaletea maendeleo wananchi wa  Mkoa wa Shinyanga na nchi nzima.

Programu hiyo Imezinduliwa leo Alhamisi Septemba 7,2023 na Mhe. Lucy Mayenga Jijini Dodoma baada ya Makatibu na Wenyeviti wa UWT  kutoka Kata 112 kutoka wilaya ya Kahama kuwasili  Mkoani Dodoma kwa mwaliko wa Mhe. Lucy Mayenga  ambapo wakiwa Jijini Dodoma Viongozi hao wamepata nafasi ya kutembelea Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.


Tukio la uzinduzi wa Programu hiyo pia limehudhuriwa na viongozi wengine wakiwemo Mbunge wa jimbo la Msalala, Mhe. Idd Kassim, Mbunge wa Jimbo la Kahama Mhe. Jumanne Kishimba,   Mbunge wa jimbo la Ushetu, Mhe. Emmanuel Cherehani, Mbunge wa Viti Maalum Chadema Mhe. Salome Makamba,  Naibu Waziri wa Nishati, Mhe. Judith Kapinga ,Mbunge wa Viti Maalum Mtwara Mhe. Agnes Hokororo  na Mbunge wa jimbo la Nyang'wale Mhe. Hussein Nassor.


Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: +255 621 896 990

Pages