Breaking

Monday, 11 September 2023

KIONGOZI WA MWENGE WA UHURU AZINDUA MRADI WA MAJI KIBAONI WILAYANI MBARALI

Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa -2023 ndugu Abdullah Shaib Kaim amezindua Mradi wa Maji wa Kibaoni Wilayani Mbarali Mkoani Mbeya na kusema kuwa anaishukru Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa utekelezaji miradi mingi ya maendeleo ikiwemo miradi wa maji.

Pia, amewashukru wadau ambao wameweza kushirikiana na Serikali kwa kutekeleza mradi wa maji wa Kibaoni.

Mheshimiwa Mhandisi Maryprisca Mahundi amesema kuwa mradi huu wa Kibaoni umejengwa kwa lengo la kuhudumia wananchi wa vijiji viwili vya kibaoni na Ihani.

Hata hivyo katika kuhakikisha kuwa mradi huu unakuwa endelevu, wananchi waendelea kutunza vyanzo vya maji, miundombinu ya maji pamoja na mazingira kwa ujumla " amesema"

Sambamba na kuzindua kwa mradi huo, Mwenge wa uhuru wa Kitaifa-2023 umeweza kutembelea chanzo cha maji cha Itamboleo pamoja na kupanda miti rafiki kwa mazingira ili kuweza kuhifadhi na kulinda chanzo cha maji cha Itamboleo.

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: +255 621 896 990

Pages