Breaking

Friday, 29 September 2023

KIHENZILE AIPONGEZA NIT KUANZISHA KITUO CHA UKAGUZI WA MAGARI

NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM

NAIBU Waziri wa Uchukuzi, David Kihenzile amefanya ziara na kukagua Miradi mbalimbali katika Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT) na kutoa maelekezo kwa taasisi za umma na binafsi kufanya ukaguzi wa magari yao ili kupunguza matukio ya ajali za barabarani.

Ametoa Maelekezo hayo mara baada ya kutembelea moja ya Kituo cha kukagulia Magari (NIT) wakati alipofanya ziara leo Septemba 29,2023 na kutembelea Miradi mbalimbali katika Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT) Jijini Dar es Salaam

Amesema ni jambo zuri kwa chuo hicho kuanzisha Kituo cha ukaguzi wa magari kwani idadi ya magari yaliyopo nchini ni zaidi ya milioni 2.5 huku Dar es Salaam ikiwa na nusu ya magari hayo.

"Ni wakati wa kutumia miundombinu hii kukagua magari kabla ya kuanza kutumika ili yawe na ubora. Naelekeza mamlaka zinazosimamia vyombo vya usafiri kuhakikisha zinakaza nati kwa lengo la kunusuru maisha ya watu wasio na hatia na nguvu kazi ya taifa," amesema Kihenzile.

Aidha amekielekeza Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT) kuanzisha vituo vingi katika maeneo mbalimbali nchini kwa ajili ya kuongeza ufanisi katika ukaguzi wa magari.
Pamoja na hayo Naibu Waziri Kihenzile ameelekeza NIT kukamilisha miradi yote kwa muda uliopangwa sambamba na kuhakikisha thamani ya fedha.

Ameelekeza NIT waongeze hosteli nyingi ili kuchukua wanafunzi wengi na kupunguza changamoto ya wanafunzi kupanga nje ya shule ambako hakuna mazingira rafiki.

Kwa upande wake, Mkuu wa chuo hicho, Prof. Zakaria Mganilwa amesema kituo cha ukaguzi wa magari kilijengwa kwa ajili ya wanafunzi wao, maofisa wa polisi wanaohusika na ukaguzi na maofisa wa bima.

Amesema wanachokifanya maofisa wa bima ni kuthamanisha gari baada ya kupata ajali na kisha kuwalipa wateja wao.

"Tumekuwa tukihamasisha umma walete magari yao Ili kujua ubora wake kwani tunakagua zaidi ya mifumo 15 hasa inayoendana na usalama wa gari,''amefafanua.

Prof. Mganilwa amesema watu ambao wanauziana magari pia Wana wajibu wa kupeleka magari hayo kufanyiwa ukaguzi kabla ya kununua ili likaguliwe na watapewa taarifa ya gari husika.

"Baada ya ukaguzi tutatoa ripoti ambayo huenda mnunuzi badala ya kununua kwa Shilingi milioni nane unaweza kuambiwa gari inahitaji matengenezo ya milioni 12 hivyo ukajikuta unanunua gari kwa milioni 20," amesisitiza.

Amesisitiza kuwa wanahamasisha watanzania watumie kituo hicho kwani ukaguzi wa gari dogo huanzia Sh 60,000 huku gharama ya magari makubwa hutegemea na mahitaji na kwamba kituo hicho kitawasaidia kuwa na uhakika wa kupunguza ajali za barabarani.

Kuhusu usimamizi wa miradi, wana miradi ya ujenzi wa majengo ya kufundishia pamoja na hosteli na kwamba watahakikisha miradi hiyo inamalizika kwa muda uliopangwa na ubora unaotakiwa.
Naibu Waziri wa Uchukuzi, David Kihenzile akiwa katika kituo cha kukagulia Magari (NIT) mara baada ya kutembelea Miradi mbalimbali ya Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT) leo Septemba 29,2023 Jijini Dar es Salaam
Naibu Waziri wa Uchukuzi, David Kihenzile akimsikiliza Msimamizi wa Kituo cha kukagulia Magari (NIT) Mhandisi Christian Nabora mara baada ya kutembelea Miradi mbalimbali ya Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT) leo Septemba 29,2023 Jijini Dar es Salaam

Naibu Waziri wa Uchukuzi, David Kihenzile akimsikiliza Mkaguzi wa magari Bw.Abel Masanja mara baada ya kutembelea Miradi mbalimbali ya Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT) leo Septemba 29,2023 Jijini Dar es Salaam
Naibu Waziri wa Uchukuzi, David Kihenzile akimsikiliza Msimamizi wa Kituo cha kukagulia Magari (NIT) Mhandisi Christian Nabora mara baada ya kutembelea Miradi mbalimbali ya Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT) leo Septemba 29,2023 Jijini Dar es Salaam
Naibu Waziri wa Uchukuzi, David Kihenzile akimsikiliza Mwalimu wa wahudumu wa ndege (NIT), Bw.Denis Mwageni mara baada ya kutembelea Miradi mbalimbali ya Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT) leo Septemba 29,2023 Jijini Dar es Salaam
Naibu Waziri wa Uchukuzi, David Kihenzile akimsikiliza Mhandisi Lameck Lugeiyamu akimuelezea namna mradi wa ujenzi wa mabweni ya wanafunzi NIT unavyoendelea mara baada ya kutembelea Miradi mbalimbali ya Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT) leo Septemba 29,2023 Jijini Dar es Salaam
Naibu Waziri wa Uchukuzi, David Kihenzile akimsikiliza Mkufunzi NIT anayesimamia Miradi ya Ujenzi (NIT), Mhandisi Juma Ngoda wakati akimuonesha ramani ya ujenzi wa miradi mbalimbali inayoendelea mara baada ya kutembelea Miradi mbalimbali ya Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT) leo Septemba 29,2023 Jijini Dar es Salaam
Naibu Waziri wa Uchukuzi, David Kihenzile akimsikiliza Mhandisi mkufunzi Hamadi Makame akielezea na kumuonesha vifaa vinavyosaidia ndege kuruka mara baada ya kutembelea Miradi mbalimbali ya Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT) leo Septemba 29,2023 Jijini Dar es Salaam

Naibu Waziri wa Uchukuzi, David Kihenzile akimsikiliza Mhandisi mkufunzi Hamadi Makame akielezea na kumuonesha Piston Engine ambayo inasaidia ndege kuwaka na kuruka mara baada ya kutembelea Miradi mbalimbali ya Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT) leo Septemba 29,2023 Jijini Dar es Salaam.
Naibu Waziri wa Uchukuzi, David Kihenzile akiwa kwenye chumba cha mafunzo ya uendeshaji ndege mara baada ya kutembelea Miradi mbalimbali ya Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT) leo Septemba 29,2023 Jijini Dar es Salaam

(PICHA ZOTE NA EMMANUEL MBATILO)
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: +255 621 896 990

Pages