Naibu Waziri Wizara ya Viwanda na Biashara Mhe. Exaud Kigahe ameridhishwa na maendeleo ya ujenzi wa jengo la Metrology Annex unaendelea katika Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE) Kampasi ya Dar es Salaam.
Hayo yamebainishwa wakati wa ziara ya kikazi iliyofanyika tarehe 26 Septemba, 2023 ambapo ilielezwa kuwa jengo hilo litagharimu kiasi cha Shilingi Bilioni 22.4, litakapokamilika litakuwa la ghorofa 10.