#Tanzania Yapongezwa Utekelezaji Mradi wa Hakimiliki Nchini
***
Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara Dkt. Hashil Abdallah (kushoto) amekutana na kufanya mazungumzo na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia kulinda hakimiliki za Ubunifu duniani -WIPO Bw. Daren Tang ( Kulia) makao makuu ya Shirika hilo Mjini Geneva, Uswisi, tarehe 13 Septemba,2023.
Mazungumzo yao yalilenga kuimarisha ulinzi wa haki miliki za ubunifu na ushirikiano wa kimataifa ambapo Dkt. Abdallah amemshukuru Bw. Tang kwa ushirikiano Mkubwa ambao WIPO imekuwa ikiutoa, ikiwemo ushauri wa kitaalamu kuhusu uanzishwaji wa Sera ya Taifa ya haki miliki na ubunifu Tanzania bara, kuanzishwa kwa sera ya haki miliki na ubunifu Zanzibar na kuanzishwa kwa Chuo cha Taifa cha Usafirishaji nchini Tanzania.
Bw. Tang ameipongeza Tanzania kwa mafanikio makubwa katika utekelezaji wa mradi wa hakimiliki nchini