Breaking

Saturday, 23 September 2023

DAWASA YAJIBU HOJA YA WAKAZI TABATA KISUKURU

--Yaainisha mipango ya muda mrefu na mfupi ya upatikanaji huduma ya majisafi.

Mamlaka ya Majisafi ya Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) imetoa uhakika wa upatikanaji wa huduma ya maji kwa wananchi wa Tabata Kisukuru na Kinyerezi, Kifuru, Kibaga na Zimbili na Kanga kwa kuainisha mipango ya muda mfupi na ya muda mrefu itakayoenda kuboresha huduma ya Majisafi kwenye maeneo hayo.

Akiongea katika kikao cha Wananchi wa eneo la Kisukuru Sabasa, Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa DAWASA, Ndugu Kiula Kingu ameeleza mipango mbalimbali iliyopo ya Serikali ya kuboresha upatikanaji wa huduma ikiwemo kuweka vituo vya kusukuma maji ili kusambaza maji kwa kasi na kufika kwa wananchi wote.

“Serikali kupitia DAWASA imekuja na mipango ya muda mfupi ya kuboresha upatikanaji wa maji, ambapo kwanza ni kuweka vituo vya kusukuma maji maeneo ya Bonyokwa na eneo la Kingazi B vitakavyosaidia kusukuma maji na kupeleka kwenye maeneo yenye miinuko," amesema Mkurugenzi Kingu.

Alibainisha pia mipango ya muda mrefu ikiwa ni pamoja na utekelezaji wa mradi wa maji Bangulo ambao utasainiwa mapema mwezi ujao ambao utakuwa ni suluhisho la kudumu na utaenda kuhudumia maeneo ya kwembe, Kinyerezi, Ukonga, Bonyokwa, Saranga, Kisukuru na maeneo ya jirani Pugu ambao utagharimu Shilingi Bilion 40.

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: +255 621 896 990

Pages