Habari njema kwa wakazi wa Kerege hadi Vikawe, kuwa ofisi ya DAWASA - MAPINGA inaendelea na zoezi la utoaji wa vifaa vya maunganisho mapya ya huduma ya majisafi kwa wateja wake.
Zaidi ya wateja 40 wa maeneo ya Kerege, Mtambani, Kiharaka, Kiembeni, Kimele na Vikawe wamepatiwa vifaa vya maunganisho mapya ya majisafi.
Zoezi la utoaji wa vifaa vya maunganisho mapya lilienda sambamba na utoaji wa elimu ya utunzaji wa miundombinu ya vifaa vya majisafi, matumizi sahihi ya maji, njia za mawasiliano pamoja na huduma nyingine zitolewazo na DAWASA.
Kwa msaada na taarifa zaidi wasiliana nasi kupitia kituo cha huduma kwa wateja namba 0800110064 (Bure) au 0734 359 622 (DAWASA - Mapinga).