Na Kadama Malunde – Malunde 1 blog
Benki ya NMB imeendesha Warsha ya Siku ya Walimu Katika Wilaya ya Kahama Mkoani Shinyanga kwa ajili ya kutambua mahusiano mazuri yaliyopo kati ya walimu na Benki ya NMB, kutambua mchango wa walimu katika maendeleo ya Benki hiyo pamoja na kuwapa fursa ya kutoa maoni na mapendezo ya namna gani wanaweza kunufaika zaidi na huduma za Benki ya NMB.
Warsha hiyo imefanyika leo Jumatatu Septemba 18,2023 Mjini Kahama ikiongozwa na kauli mbiu ‘Mwalimu Spesho – Umetufunza Tunakutunza’ ambapo mgeni rasmi alikuwa Afisa Tarafa Kahama Mjini, Julius Chagama kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya ya Kahama Mhe. Mboni Mhita.
Kupitia warsha hiyo walimu wamejifunza masuala ya Kibenki ikiwemo mikopo,bima,amana na huduma mbalimbali za NMB zitakazowasaidia kupanua uwezo wao kiuchumi na kujenga utamaduni wa kuweka akiba ili kukidhi mahitaji ya dharura pindi yanapojitokeza.
Akizungumza wakati wa Warsha hiyo, Julius Chagama ameipongeza Benki ya NMB kwa kuandaa Warsha ya Siku ya Walimu akisema jitihada hizo za Benki ya NMB ni nzuri na zinaunga mkono juhudi za Serikali ya awamu ya Sita chini ya Uongozi thabiti wa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika kuhakikisha Watanzania walio wengi wanajumuishwa katika mfumo rasmi wa kifedha ili kuinua vipato vyao na uchumi kwa ujumla.
“Nawapongeza sana NMB kwa bidhaa za akiba na mikopo inayolenga mahitaji ya kila makundi ya wateja kama walimu na jamii kwa ujumla. Tunawapongeza kwa kujali mahitaji ya wafanyakazi kwani mikopo hii imekuwa msaada sana katika kukidhi mahitaji mbalimbali katika ngazi ya familia n ahata kufanikisha maandalizi yao kwa Maisha ya baadae pale wanapostaafu”,amesema.
Afisa Tarafa Kahama Mjini, Julius Chagama akitoa hotuba kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya ya Kahama Mhe. Mboni Mhita wakati wa Warsha ya Siku ya Walimu Katika Wilaya ya Kahama Mkoani Shinyanga iliyoandaliwa na Benki ya NMB
Katika hatua nyingine, Chagama amewahamasisha walimu na watumishi wengine wa serikali watumie taasisi rasmi zinazotoa mikopo rasmi ikiwemo Benki ya NMB ili kuepukana na mikopo umiza ‘Kausha Damu’ inayotolewa kwenye makampuni binafsi ambayo imekuwa ikiwaathiri zaidi walimu.
“Ofisi ya Mkuu wa Wilaya imekuwa ikipokea kesi nyingi za migogoro kati ya walimu na wakopeshaji wa makampuni binafsi. Walimu wamekuwa waathirika wakubwa wa mikopo umiza ‘kausha damu’, unakuta mwalimu kakopa, anamaliza deni lakini bado anaendelea kukatwa pesa zake. Benki hii ya NMB inaenda kutuweka katika mikono salama ya mikopo salama. Watumishi tumieni Benki ya NMB kupata mikopo rasmi”,ameongeza Chagama.
“Natoa rai kwa Benki ya NMB kuzidi kuboresha huduma kwa wateja hasa walimu ili idadi yao iweze kuongezeka jambo ambalo litawapa fursa nyingi zikiwemo kukopa ili wawe na amani wanapokuwa kazini na kuongeza tija kwenye maeneo yao ya kazi. Pia endeleni kubuni bidhaa, huduma na program nyingi si kwa ajili ya walimu tu, hata kwa watumishi na wafanyakazi wa kawaida waweze kumudu”,ameongeza Chagama.
Kwa upande wake, Meneja wa Benki ya NMB Kanda ya Magharibi, Seka Urio amewashukuru Walimu kwa kuendelea kuwa wateja wazuri huku akiwahamasisha kupata mikopoyenye masharti nafuu kupitia benki ya NMB.
“Leo tumekutana na walimu zaidi ya 250 kutoka Halmashauri ya Msalala, Ushetu na Manispaa ya Kahama katika Warsha ya Siku ya Walimu ili kuwaonesha kwa kina na upana fursa zinazotolewa katika Benki ya NMB. Tulizindua mpango huu mwaka 2022 ili kuwaonesha walimu namna ya kupata mikopo yenye riba nafuu ili kuepukana na mikopo umiza na kuhakikisha Benki ya NMB inaendelea kuwa suluhisho kwa watanzania”,amesema Urio.
“Benki ya NMB inatoa mikopo yenye masharti nafuu. Walimu ni miongoni mwa wateja wetu wengi,na ni kundi ambalo limekuwa kundi lengwa kwa mikopo umiza na wamekuwa waathirika wakubwa wa mikopo ya kausha damu, kausha maji kutokana na kwamba wamekuwa wakikopo kwenye makampuni binafsi na kutozwa riba kubwa na masharti magumu hali inayosababisha kuwa na msongo wa mawazo ‘Stress’ kuhusu mikopo hiyo”,ameongeza Urio.
Meneja Mwandamizi wa Mauzo wa Benki ya NMB kutoka Makao Makuu, Isaac Mgwassa amesema Benki ya NMB ni benki ya Kwanza miongoni mwa taasisi nyingi za fedha nchini kufikiria kuandaa siku maalumu kwa ajili ya walimu lengo likiwa ni kuwafikia walimu zaidi ya 9000 nchini hivyo itaendelea kuwatunza walimu kwa masuluhisho mbalimbali ya kifedha.
Kwa upande wao, walimu waliopata mafunzo hayo akiwemo Tegemeo Severiani, Levina Kassim na Regina Mbozu wameishukuru Benki ya NMB kwa kuandaa warsha hiyo ambayo imekuwa fursa nzuri kujua namna gani wanaweza kupata huduma zinazotolewa na benki hiyo kwa unafuu, uharaka na ufanisi lakini pia kuepukana na mikopo umiza ambayo imekuwa ikisababisha walimu wapunguze ufanisi wa kazi zao.
ANGALIA PICHA HAPA CHINI
Afisa Tarafa Kahama Mjini, Julius Chagama akitoa hotuba kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya ya Kahama Mhe. Mboni Mhita wakati wa Warsha ya Siku ya Walimu Katika Wilaya ya Kahama Mkoani Shinyanga iliyoandaliwa na Benki ya NMB leo Jumatatu Septemba 18,2023 . Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Afisa Tarafa Kahama Mjini, Julius Chagama akitoa hotuba kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya ya Kahama Mhe. Mboni Mhita wakati wa Warsha ya Siku ya Walimu Katika Wilaya ya Kahama Mkoani Shinyanga iliyoandaliwa na Benki ya NMB
Meneja wa Benki ya NMB Kanda ya Magharibi, Seka Urio akizungumza kwenye Warsha ya Siku ya Walimu Katika Wilaya ya Kahama Mkoani Shinyanga iliyoandaliwa na Benki ya NMB
Meneja Mwandamizi wa Mauzo wa Benki ya NMB kutoka Makao Makuu, Isaac Mgwassa akizungumza kwenye Warsha ya Siku ya Walimu Katika Wilaya ya Kahama Mkoani Shinyanga iliyoandaliwa na Benki ya NMB
Meneja Mwandamizi wa Mauzo wa Benki ya NMB kutoka Makao Makuu, Isaac Mgwassa akizungumza kwenye Warsha ya Siku ya Walimu Katika Wilaya ya Kahama Mkoani Shinyanga iliyoandaliwa na Benki ya NMB
Kaimu Afisa Elimu Msingi Halmashauri ya Manispaa ya Kahama, Sadick Juma Kigaile akizungumza kwenye Warsha ya Siku ya Walimu Katika Wilaya ya Kahama Mkoani Shinyanga iliyoandaliwa na Benki ya NMB
Afisa Elimu Halmashauri ya Msalala, Hajra Mmkoki akizungumza kwenye Warsha ya Siku ya Walimu Katika Wilaya ya Kahama Mkoani Shinyanga iliyoandaliwa na Benki ya NMB
Meneja wa Benki ya NMB Tawi la Kahama, Godfrey Mkumbo akizungumza kwenye Warsha ya Siku ya Walimu Katika Wilaya ya Kahama Mkoani Shinyanga iliyoandaliwa na Benki ya NMB

Walimu wakiwa kwenye Warsha ya Siku ya Walimu katika Wilaya ya Kahama iliyoandaliwa na Benki ya NMB

Huduma za Kibenki zikitolewa kwenye Warsha ya Siku ya Walimu katika Wilaya ya Kahama iliyoandaliwa na Benki ya NMB