Kazi ya uchimbaji na ulazaji wa bomba za mtandao wa majitaka za ukubwa wa inchi 10 ikiendelea eneo la Sinza Mori Jijini Dar es Salaam, ambao ni sehemu ya utekelezaji wa mradi wa Usafi wa Mazingira PSSSF Sinza - Kijitonyama.
Utekelezaji wa mradi huu unaotekelezwa na Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) na sasa umefikia asilimia 30 na unategemewa kukamilika ifikapo mwishoni mwa mwezi Septemba 2023 na kunufaisha zaidi ya wateja 1000.