Breaking

Monday, 14 August 2023

WIZARA, WADAU WA MADINI WATEMBELEA SOKO LA KIMATAIFA YIWU CHINA



Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Madini Msafiri Mbibo akiambatana na Rais wa Shirikisho la Vyama Vya Wachimbaji Tanzania (FEMATA) John Bina pamoja na ujumbe wa wadau wa madini, leo Agosti 14, 2023 wametembelea Soko la Kimataifa la Yiwu nchini China kujionea bidhaa mbalimbali zinazozalishwa kwa kutumia madini ikiwa ni sehemu ya kujifunza.

Bidhaa hizo ni pamoja na vito, vifaa vya umeme ikiwemo magari, vyombo na mapambo ya ndani.

Safari ya wadau wa madini nchini China inajumuisha wafanyabiashara wa madini, wachimbaji na watoa huduma migodini .

Aidha, mbali na wadau hao, pia, watendaji wa taasisi chini ya wizara pamoja na taasisi za fedha wanashiriki katika ziara hiyo.


Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: +255 621 896 990

Pages