Breaking

Thursday 3 August 2023

WAZIRI MKUU AIAGIZA TPA KUTEKELEZA MPANGO WA MIUNDOMBINU YA BIDHAA

- APONGEZA MABORESHO HUDUMA TPA

MAMLAKA Ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA,) imepongezwa kwa jitihada zinazoendelea kufanyika ili kuboresha huduma za Bandari ili kukidhi mahitaji ya Soko la ndani na Nchi jirani.

Waziri Mkuu Majaliwa ametoa pongezi hizo alipotembelea Banda la TPA katika maonesho ya kimataifa ya Wakulima- Nanenane 2023 yanayoendelea katika Viwanja vya John Mwakangale Mkoani Mbeya.

Pamoja na pongezi hizo, Mhe. Majaliwa ameilekeza Menejimenti ya TPA kutekeleza kwa haraka mpango wake wa kuwa na miundombinu ya kuhifadhia bidhaa zinazoharibika haraka [ Cold rooms] ili kuongeza tija katika Sekta za Kilimo hasa cha matunda na mbogamboga, mazao ya Mifugo na Uvuvi.

Akimkaribisha Mhe. Waziri Mkuu kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa TPA Bw. Plasduce Mbossa, Meneja Uhusiano na Mawasiliano wa TPA Bw. Nicodemus Mushi amesema, TPA inathamini sana mchango wa Sekta ya Kilimo katika kiwango cha shehena zinazohudumiwa na TPA ambapo, pembejeo za kilimo zinazokwenda kwa Wakulima na mazao ya kilimo kwenda katika masoko ya kitaifa na kimataifa hutegemea huduma za bandari katika usafirishaji wake.

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: +255 621 896 990

Pages